• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Wachimbaji wadogo wa madini kata ya Ntwike wilayani Iramba wachangia madawati 225 kuunga mkono jitihada za serikali.

Posted on: January 5th, 2019

Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amekabidhiwa madawati 225 kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo katika Mgodi wa Sekenke Nkonkilangi Wilaya ya Iramba kwa ajili ya shule za sekondari na misingi wilayani Iramba ili kuunga mkono jitihada za serikali.

 Akizungumza na wachimbaji wadogo katika machimbo ya Sekenke yaliyopo katika Kijiji cha Nkonkilanga, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilayani Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewashukuru sana kwa ushirikiano wao na kwa kujitoa kuchangia madawati.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewaomba wachimbaji wadogo wadogo kuifadhi na kutunza mazingira ili yawe mazuri kwa lengo la kuepukana na Magonjwa ya milipuko.

Makundi ya wachimbaji waliochangia madawati ni Sekenke One Madawati 30, Iramba Nkulu Madawati 65, Iramba Kenkang’ombe Madawati 20, Uwema-Mzizini Madawati 10, Malaki-Uwaseke Madawati 20, Nassoro Plant Madawati 50, Maulid Plant Madawati 10 na Waziri Illution Madawati 20.

Vile vile Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa wale ambao wanawaomba Rushwa. “Suala la Rushwa halina mjadala, Rushwa ni adui wa haki, usikubali kununua haki yako, wananchi mnaombwa Rushwa lakini hamtoi taarifa, wananchi toa taarifa ili tuwakamate hao waarifu” alisema Mhe Luhahula

Afisa TAKUKURU wilaya ya Iramba Ndugu Benjamin Masyaga alisema Rushwa ni tatizo ambalo athari zake zinamgusa kila mwananchi. Tatizo hili linasababisha jamii kukosa imani na Serikali yao, amani baina ya wanajamii, kujenga matabaka ya walionacho na wasiokuwa nacho. Vilevile rushwa imekuwa chanzo cha kudhoofisha huduma zinazotolewa katika jamii. “kila mwananchi sehemu alipo aweze kushiriki kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa bila kuchukua muda mrefu. Kila mwananchi anawajibika kuzuia vitendo vya rushwa na kutoa taarifa hizo ili kuchukuliwa hatua stahili za kisheria dhidi ya wala Rushwa na kutokomeza Rushwa nchini.

Ametoa wito wa kukataa kujihusisha na vitendo vya Rushwa ikiwemo kutoa au kupokea Rushwa na kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya Rushwa katika ofisi za TAKUKURU zilizo wilayani Iramba au kwa kupiga simu ya bure namba 113 au kwa vyombo vingine vya dola na viongozi wanaohusika.

Ameongeza kusema wananchi watoe ushirikiano kwa TAKUKURU na vyombo vingine vya dola na kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya Rushwa kwakuwa mara nyingi TAKUKURU imekuwa ikishindwa kufikia malengo kutokana na wananchi kutotaka kutoa ushirikiano

Mkurugenzi wa uhamiaji wilayani Iramba Ndg. Doto Selesini amewataka wananchi wa wilaya ya Iramba kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu ili kuthibiti raia wa kigeni na yeyote atayebainika kuficha wahamiaji haramu kwenye eneo lake atachukuliwa hatua kali za kisheria. Alitoa wito huo kwa wananchi kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka watoe taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogudua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.

Picha za madawati yaliyopokelewa na mkuu wa wilaya Iramba


Madawati yaliyochangiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo IRAMBA KENKANG'OMBE mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 20.

Madawati ya kikundi cha wachimbaji wadogo MAULID PLANT mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 10.

Madawati yaliyochangiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo  UWEMA MZIZINI katika mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 10.



Tangazo

  • PATA TAARIFA ZA SERIKALI KILA SIKU KIGANJANI MWAKO January 22, 2019
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA. January 24, 2019
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2018 HALMASHAURI YA WILAYA IRAMBA January 05, 2019
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2018 January 05, 2019
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • Ushirika wa wachimbaji madini wa kisonga shelui (UWAWAKISHE) kata ya Mgongo wilayani Iramba wachangia madawati 60 katika shule ya sekondari Mgongo kuunga mkono jitihada za serikali.

    February 18, 2019
  • Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba (Diwani wa CCM kata ya Urughu) Mhe: Simion Tyosera ameendesha kikao cha Baraza la Madiwani wilayani hapa na kujadili mambo mbalimbali.

    February 14, 2019
  • Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Pro. Makame Mbarawa amefanya ziara ya kukagua uchimbaji wa visima 3 vya maji kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida.

    February 12, 2019
  • Kamati ya fedha, Mipango na utawala wilaya ya Iramba imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Iramba mkoani Singida.

    February 06, 2019
  • Angalia Zaidi

Video

SHANGWE ZA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU WILAYANI IRAMBA.
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.