TAARIFA YA IDARA YA FEDHA NA BIASHARA
Idaraya fedha ni idara inayojishughulisha na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato namatumizi ya fedha katika halmashauri, na kutoa ushauri wa namna bora yamatumizi ya fedha.
Katikakusimamia huko inahakikisha kunakuwa na mfumo thabiti wa udhibiti wandani(lnternal control system)Ambao pamoja na kuzingatia masuala ya kiutendajipia unalenga katika kuangazia taratibu nzima za kifedha za halmashauri,Lakinipia ina kazi ya kuwasilisha taratibu za kifedha kwenye kamati ya fedha kwaajili ya mapitio,pia kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha wa mali zahalmashauri pamoja ne fedha, hii ikiwa ni kuwa na mpango kazi mzuri wawafanyakazi na utawala ndani ya idara ya fedha,Nakuishauri halmashauri katikamasuala yote yanayohusuyo mambo ya fedha.
Idaraya fedha ina jumla ya vitengo 4, Ambavyo ni: Kitengo cha mishahara, kitengo chamapato, kitengo cha matumizi, na kitengo cha taarifa za mwisho za mahesabu yahalmashauri (Final account), Kazi za vitengo hivyo ni kama ifuatavyo;
I: MATUMIZI
(i)Kuandaamalipo yote
(ii)KuandaaBajeti ya matumizi ya kawaida,
(iii)Kuhakikishauwepo wa nyaraka zote za malipo kabla na baada ya kulipa, (iv)Kuhakikishataratibu na sheria za kifedha zinatekelezwa,
(v)kuhakikishakuwepo na majalada ya kumbukumbu kwa malipo yaliyolipwa,
(vi)Kufanyausaili wa kimahesabu kati ya benki na vitabu vya kumbukumbu vya halmashauri.
(vi)Kuandaataarifa za fedha na kuziwasilisha sehemu husika kwa wakati.
2: MAPATO
(i)Kuhakikishainakusanya mapato yote ya halmashauri,
(ii)Kuhakikishakuna udhibiti mzuri wa mapato ya Halmashauri,
(iii)Kupelekafedha taslimu na hundi benki
(iv)Kuandaaripoti mbalimbali na kuziwasilisha sehemu husika, (v)Kuweka utaratibu rahisi wamalipo ya fedha taslimu kwa wateja,
(vi)Kubunivyanzo vipya vya mapato,
3: MlSHAHARA
(l)Kuandaaorodha ya watumishi kwa ajili ya kulipwa mishahara
(ii)Kutunzaorodha ya watumishi wanaolipwa mishahara na kutunza kumbukumbu za makatoyakatwayo watumishi kwenye mishahara yao
(iii)Kuandaabajeti ya mishahara kwa watumishi
(iv)Kuandaataarifa mbalimbali za mishahara na kupeleka sehemu husika
(v)Kushughulikiamatatizo yote ya mishahara inayotokea kwa watumishi
4: KITENGO CHA TAARIFA ZA KIMAHESABU (Final account)
(i)Kuandaausuluhisho wa taarifa za cashbook zinatunzwa halimashauri na zile zilizopobenki
(ii)Kujibu hoja za ukaguzi (iii)Kuanda taarifa za mapato na matumizi
(iv)Kutunzacashbook.
Idaraya fedha ina jumla ya wataalamu 9 ambao wako makao makuu ya Halmashauri.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.