Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameagiza Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kutumia ubunifu, Weledi pamoja na busara katika kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiowaadilifu na kuwachukulia hatua wale wasiotoa risiti za EFD.
Mwenda amebainisha hayo katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya kilichoketi Januari 29,2024 na kusisitiza kuwa mfanyabiashara yeyote atakaye bainika kuendelea kukiuka kulipa kodi taarifa iwasilishwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Amesema suala la ulipaji kodi ni wajibu wa kila mwananchi kisheria ili kusaidia Serikali kupanga shughuli za kuwaletea wananchi wake maendeleo, akihimiza TRA kuwa wabunifu katika ukusanyaji mapato na kufanya operesheni za mara kwa mara kwa wafanyabiashara wote wilayani humo.
“TRA fanyeni operesheni za mara kwa mara kwa wafanyabiashara wote ambao wapo ndani ya Wilaya ya Iramba na wanaostahili kutumia mashine za Kielektroniki (EFD) basi wanakuwa nazo na kwa wale ambao watakuwa wakaidi baada ya kuwafuatilia na kuwapa elimu basi sheria iweze kuchukua mkondo wake juu yao kwani hao ni wahujumu Uchumi wa Serikali”. Amesisitiza DC Mwenda.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Wilaya ya Iramba CPA Iddi Omari amesema ufanisi wa utendaji unatokana kuratibu Mafunzo na Elimu kwa Mlipa kodi semina zaidi ya 9 zimefanyika na kuwatembelea Wafanyabiashara katika biashara zao kusisitiza utoaji wa risiti za kielektroniki, ulipaji wa kodi kwa wakati pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto za kibiashara, pia kupata maoni ya kuboresha biashara zao.
Kwa Mwaka wa fedha 2023/24 TRA Wilaya ya Iramba ilikusanya Shilingi Bilioni 1.3 (1,356,780,560) sawa na ongezeko la asilimia 136% ya lengo Tzs. 1,000,000,000.
Katika kipindi cha Mwezi Julai 2024 hadi Disemba 2024 imekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 (1,560,731,319.45) sawa na ufanisi wa asilimia 125% ya lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 1.2 (1,234,568,517).
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.