
DC MWENDA APOKEA MWENGE WA UHURU IRAMBA, KUZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA BILIONI 5.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Mhe. Suleiman Mwenda leo Jumanne Julai 09, 2024 ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe Mkoani hapa.
DC Mwenda ameupokea Mwenge huo wa Uhuru leo katika kijiji cha Maluga wilayani hapa huku akiahidi kuulinda na kuukimbiza kilometa 68.1 ukiwa unawaka, unangaa na kumeremeta kwa muda wote utakaokuwepo Iramba.
Aidha, amedokeza kuwa unatembelea, kuona, kuweka mawe ya msingi, kupata taarifa mbalimbali ikiwemo kuizindua miradi saba yenye thamani ya sh bilioni 5.084 ambazo zilitolewa na serikali anayoiongoza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
"Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hakika ameitendea haki wilaya yetu kwa sababu katika kila kata kati ya kata 20 za Wilaya hii kuna miradi mikubwa yenye kugharimu fedha nyingi, asante sana Rais wetu," ameshukuru Mwenda.


KIOMBOI, IRAMBA
Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Telephone: 026 - 2532253
Mobile: 026 - 2533001
Email: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.