• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

KONGAMANO LA ELIMU LATOKA NA MAAZIMIO ILI KUPANDISHA UFAULU

Posted on: December 3rd, 2021

KONGAMANO la elimu wilayani Iramba limefanyika leo Tarehe 3.11.2021. Katika kujadiliana kwenye agenda hii, muongozo wa maaswali mawili ulitumika kuongoza majadiliano ambayo yamefanyika katika makundi mawili kama ifuatavyo.

Swali la Kwanza: Nini sababu za kutofikia malengo ya 90% katika ufaulu?

Swali la pili: Nini kifanyike ili tufikie malengo ya ufaulu wa 90%?

Kabla ya wawasilishaji wa makundi haya mawili, mwenyekiti alimkaribisha mkuu wa shule ya st. Desderius kwa ajili ya kuelezea kwa ufupi sababu zinazopelekea shule hiyo kufaulu na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya, Mwalimu aliezea kuwa sababu zinazopelekea kuwa na ufaulu mzuri ni pamoja na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia, walimu kufanya kazi kwa moyo na kwa kujituma, uwepo wa vitendea kazi muda wote katika mazingira ya kujifunzia, Ushirikiano mzuri wa walimu, wazazi na jamii kwa ujumla, kuelimisha jamii ili iweze kuelewa umuhimu wa suala zima la elimu na umuhimu wake, Kumtanguliza mungu katika kila jambo ili aweze kuwakomboa Watoto katika mafundisho na mila potofu

Baada ya majadiliano katika makundi hayo makuu mawili hayo yaliyoshirikisha pia Madiwani, Viongozi wa Dini, Vyama vya siasa, Wenyeviti wa kamati za shule,wazazi,wakuu wa idara, Maafisa tarafa, Watendaji wa kata na vijiji, Taasisi mbalimbali zikiwemo SEMA, Haki Elimu, Sight saver, Wakuu wa shule za msingi na sekondari na wanafunzi, wameadhimia yafuatayo:-

  • Kuwepo kwa chakula cha mchana shuleni kwa kuwashawishi wazazi kuchangia
  • Kutoa elimu na kuishawishi jamii ili itambue umuhimu wa elimu, hivyo wazazi wawasimamie Watoto wapatae elimu na siyo kuwashawishi wafanye vibaya katika mitihani yao. Njia zinazoweza kutumika ni pamoja na kuwatumia viongozi wa serikali, Wazee maarufu, matamasha ya michezo mbali mbali, sinema na viongozi wa dini.
  • Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji iwaandikie barua watendaji wa kata na vijiji kuwakumbusha kutumia sheria kudhibiti na kutokomeza utoro wa wanafunzi kwa kuzitumia sheria hizo kutoa adhabu  kwa wanafunzi ambao ni watoro
  • Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ipeleke takwimu sahihi OR-TAMISEMI kulingana na mahitaji ya walimu yaliyopo. Ifanyike haraka mara tu baada ya vibali vya ajira kuwa vimetolewa.
  • Kukemea migogoro ya aina yeyote iwe ya walimu kwa walimu au walimu kwa viongozi lengo ni kuleta uafanisi wa kielimu.
  • Idara ya elimu kuwasilisana na uongozi wa chuo cha ualimu kinampanda  ili wakati wa mazoezi ya ufundishaji kwa vitendo(BTP) wapelekwe kwenye shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Suala hili lisimamiwe na afisa elimu Wilaya.
  • Idara ya elimu Wilaya ifanye msawazo wa ikama ya walimu ili kuleta usawa katika utendaji kazi wa walimu
  • Kuwepo kwa kambi za kitaaluma za wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwa shule za misingi na sekondari, Mkurugenzi aandike barua kupeleka kwa wahusika, kambi ziwepo mpaka  itakapokaribia mitihani.
  • Mkurugenzi awachukulie hatua za kinidhamu walimu wote wanaoishi nje ya vituo vyao vya kazi hasa viongozi(Walimu wakuu na maafisa elimu kata)
  • Ikama irekebishwe kwa kuzingatia umahiri wa walimu,
  • Maagizo ya kikao cha wadau yatolewe na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji juu ya utekelezaji wa suala la lishe shuleni
  • Kuwepo kwa ratiba rasmi ya majaribio na mitihani hasa kwa madarasa yeye mitihani
  • Walezi wa kata watembelee mara kwa mara shule zao lengo ni kubaini changamoto zilizopo na kuzitatua. Afisa Elimu wilaya asimamie
  • Shule zote za sekondari ziandaliwe utaratibu wa kuwa na mabweni ili kuwasaidia wanafunzi hasa wale wanaotoka mbali na mahali shule ilipo
  • Walimu wanaokaa nje ya vituo vya kazi watekeleze agizo hilo la kuhamia kwenye vituo vyao vya kazi na watakao kaidi basi mkurugenzi awachukulie ahatua za kinidhamu

 Mwenyekiti wa Kongamano hilo,amesema maazimio yote yatafanyiwa kazi ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa umuhimu wake.


Mwenyekiti wa Kongamano hilo, akizungumza na wadau wa elimu katika Kongamano la Elimu Wilayani Iramba.

Ofisa Elimu Idara ya elimu msingi Wilaya ya Iramba Mwl Chacha kehogo akizungumza katika Kongamano la Elimu lililofanyika Wilayani Iramba.

Kaimu Ofisa Elimu Idara ya elimu sekondari Wilaya ya Iramba Mwl Patrcia Ngaa akizungumza katika Kongamano la Elimu lililofanyika Wilayani Iramba

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ambaye ni mkuu wa idara ya utawala na utumishi ndgu B’hango J. Lyangwa akichangia katika Kongamano hilo.

Kaimu Mwenyekiti wa Halmshauri ambaye ni diwani wa kata Ulemo Mhe. Peter J. Peter akichangia maoni yake katika Kongamano hilo.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya akizungumza katika kongamano hilo.


Mdau wa elimu (Haki elimu) akichangia mada katika mkutano huo wa elimu.

Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia majadiliano katika kongamano hilo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa elimu kwenye kongamano.

Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia majadiliano katika kongamano hilo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa elimu kwenye kongamano.

Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia majadiliano katika kongamano hilo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa elimu kwenye kongamano

Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia majadiliano katika kongamano hilo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mjadala wa elimu kwenye kongamano

Wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia majadiliano katika kongamano hilo.


Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • KIDATO CHA KWANZA KURIPOTI SHULE January 13, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"

    March 24, 2025
  • DC MWENDA AWASISITIZA WALIPA KODI KUFANYA MAKADIRIO YA KODI KABLA YA MACHI 31, 2025

    March 20, 2025
  • DC MWENDA NA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA WACHANGIA JUMLA YA MADAWATI 98 SHULE YA MSINGI MSANSAO ILIYOPO KATA YA MTEKENTE

    March 10, 2025
  • WALIMU WAKUU 108 WA SHULE ZA MSINGI NA MAAFISA ELIMU KATA 20 WILAYANI IRAMBA WAPEWA MAFUNZO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI FANISI KUPITIA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA ZA WALIMU WAKUU NA MAAFISA ELIMU KATA

    March 19, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.