Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mwandisi. Jackson Masaka akiwa na Viongozi mbali mbali kutoka Singida Manispaa, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na wananchi wa kata ya Kituntu Wilayani Ikungi wameadhimisha Kilele cha wiki ya maji Kimkoa yaliyofanyika kijiji cha Ntewa Kata ya Kituntu Wilaya ya Ikungi. Kauli Mbiu “HIFADHIMAJI NA MFUMO WA KIIKOLOJIA KWA MAENDELEO YA JAMII”.
Shughuli izi za Maadhimisho ya Kilele cha wiki ya maji zimeanza kwa uzinduzi wa Kiosk cha maji katika eneo la Bima kilichojengwa na mamlaka ya maji na maji taka Singida mjini. Kiosk hiki kimeziduliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina M. Lutambi.
Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Maji ufanyika Tarehe 22/3 kila mwaka Nchini Tanzania. Aidha Asilimia ya 44.3 ya wakazi waishio vijijini katika Mkoa wa Singida wanapata huduma ya maji safi na salama. Idadi ya Vituo vya kuchotea maji,Singida Manispaa ina Idadi ya vituo 251,Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ina idadi ya vituo 719. Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ina idadi ya vituo 468, Halmashauri ya Wilaya ya Singida ina vituo 716, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ina vituo 492, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ina idadi ya vituo 127 na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ina idadi ya vituo 766,
Kaimu mkuu wa Mkoa amewapongezi waandisi wote wa Halmashauri za Wilaya zote za Mkoa wa Singida kwa kutekeleza Miradi mbali mbali ya Maji Mkoani Singida. Pia amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wa kuadhimisha kilele cha wiki ya maji Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida.
Vile Vile Amewashauri kuacha kukata miti ili kuwa namazingira bora. Amewaasa wananchi wa Kata ya kituntu kutupa shoka na kukamatamzinga kwa ajili ya kufuga nyuki ili kutunza mazingira, Kupata mvua ya kutoshapia kuifadhi mfumo wa maji kwa maendeleo ya jamii.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.