By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Afisa Mwandikishaji Wilayani Iramba imetangaza majina ya waandishi wasaidizi na BVR KIT Operator wa vituo vya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
Afisa Mwandikishaji ametangaza majina hayo leo Jumapili Oktoba 20, 2019.
Aidha Afisa mwandikishaji anawajulisha wote walioteuliwa kufika ukumbi mkubwa wa halmashauri Oktoba 23, 2019 saa mbili asubuhi.
Mafunzo na maelekezo kwa ajili ya maandalizi ya kufanya kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yatatolewa siku hiyo.
Zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliowahimiza vijana waliotimiza miaka 18 wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili kutimiza haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Waziri Mkuu alizindua zoezi hilo Julai 18, 2019 katika uwanja wa Mandela, Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
“Nitoe rai kwa vijana wote wa Kitanzania waliotimiza umri wa miaka 18 au wale ambao watatimiza umri huo ifikapo Oktoba, 2020 wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hawa ndio walengwa wakuu kwa sababu wanaingia kwa mara yakwanza katika uchaguzi.
“Ikumbukwe kuwa, bila kujiandikisha hawaweza kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.Hivyo kujiandikisha kwao kutawahakikishia ushiriki wao katika uchaguzi wa viongozi.” Alisema Waziri Mkuu
Zoezi hilo litafanyika kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo litafanyika nchi nzima na linatarajiwa kukamilika Machi, 2020.
Akiwahutubia wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliofanyika kwenye viwanja vya Mandela Mkoani Kilimanjaro Julai 18, 2019. Waziri Mkuu Majaliwa, alisema watakaohusika awamu hii ni wapiga kura waliotimiza miaka 18 hivi karibuni, wale watakaotimiza miaka 18 wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, waliohama kata au jimbo na kuhamia maeneo mengine ya kiuchaguzi.
Wengine ni waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika, wanaohitaji kuboresha taarifa zao mfano majina ambayo hapo awali yalikuwa yamekosewa sambamba na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza sifa kama vile kufariki. New Doc 2019-10-20 20.42.24.pdf New Doc 2019-10-20 20.48.16.pdf New Doc 2019-10-20 20.48.16-1.pdf
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.