Mkuu wa Wilaya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Iramba ambaye pia ni Afisa Uchaguzi Bwana. Emmanuel Makwaya wamepokea Ufadhili wa Chakula toka kwa Manase E. Kingu kwa ajili Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kimpunda.
Ndg. Manase Kingu, Mwaka Jana 2017 amefadhili chakula pamoja na Mahindi Gunia 5, Maharage Kilo 100, Mchele Kilo 300, Mafuta ya Kula Lita 40,Chumvi Katoni 1 na Sukari Kilo 100 Vyenye Gharama ya TShs 1,350,000/= kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kimpunda.
Vile vile kwa Mwaka huu 2018 Ndgu Manase amefadhili Wanafunzi wa Shule ya Kimpunda Mahindi Gunia 10, Mchele Kilo 445, Maharage Kilo 250,Mafuta ya Mboga Lita 60, Chumvi Catoni 1 na Sukari kilo 10 vyenye Gharama yaTsh2,430,000/=.
Pia amekua akifadhili viatu jozi 155, soksi jozi 155,masweta jozi 155 vyenye gharama Tshs 2,543,000/= Pamoja na Miradi mingine ya nyumba ya walimu, Bwalo la chakula, choo cha kisasa, Mradi wa maji na Kuleta Solar Power ambayo itawasaidia wanafunzi kujifunza kwa muda mwingi.
Aidha Uongozi wa Shule ya Msingi Kimpuda umemshukru Mkuu wa Wilaya kwa Ufadhili wa Mahindi Gunia 2 Kwa Ajili ya Wanafunzi katika juhudi za kuunga mkono Upatikanaji wa chakula mashuleni kama njia moja wapo ya kuinua kiwango cha taaalum shuleni hapo.
Uongozi wa shule Umemuomba Mkuu wa Wilaya kuongeza Walimu Kwenye Shule kwani kuna upungufu wa walimu pamoja na shule kuwa na wanafunzi 802 kuna walimu tisa tu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.