• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Comments |
Iramba District Council
Iramba District Council

The United Republic of Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Iramba District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Kisharita Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba.

Posted on: November 9th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Kisharita Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba.

Katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea wananchi wa wilaya ya Iramba, Mhe: Luhahula amewapongeza walimu na wananchi wa kijiji cha Kisharita kwa kuweza kupandisha ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la Saba wilayani Iramba mwaka huu.” Nawapongeza sana walimu wa wilaya ya Iramba na wazazi kwa kupeleka chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu na hatimaye kupanda kwa ufaulu wa mitihani ya Darasa la saba mwaka huu” Alisema Mhe Luhahula.

Ameongeza kusema Wanafunzi wote walifaulu mitihani yao ya Darasa la Saba lazima wajiunge na kidato cha kwanza. wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakiksiha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha watoto masomo “wazazi lazima Mhakikishe watoto wenu waliofaulu mitihani ya Darasa la Saba wanajiunga na Elimu ya sekondari pia lazima kuwalinda watoto wenu na Wakina mama waache tabia ya kuficha wanaume wanaowapa wanafunzi mimba”.

Aidha Mhe Luhahula amesisitiza wananchi kuandaa mashamba kwa wakati kwa kuhakikisha wanaunguza majani yote ili kuua wadudu walioshambulia mahindi mwaka jana.

Vile vile Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa wale ambao wanawaomba Rushwa. “Suala la Rushwa halina mjadala, Rushwa ni adui wa haki, usikubali kununua haki yako, wananchi mnaombwa Rushwa lakini hamtoi taarifa, wananchi toa taarifa ili tuwakamate hao waarifu” alisema Mhe Luhahula.

Mhe Luhahula amesisitiza kila Kaya kujenga choo bora ili kuepukana na magonjwa ya kipindupindu. Amewataka wananchi kujenga vyoo bora na ameomba viongozi wa ngazi za vijiji na kata kutoa Elimu kuhusu usafi binafsi, mazingira na kushiriki katika uzoaji takata za majumbani. “Mvua zinaanza kunyesha na vyoo vitaaza kutitia na kuanguka na kuhatarisha maisha yenu, naagiza kila kaya ijenge choo bora na atakayekaidi atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, Wale ambao hawajakamilisha kujenga vyoo wahakikishe vinajengwa na kukamilika na watakao kahidi nitawakama, wananchi hawawezi kufa kwa magonjwa yanayotokana na uchafu, operesheni itaanzishwa kwa ajili ya kubaini kaya zote ambazo hazina vyoo bora na kuchukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Mhe. Luhahula.

Mhe: Luhahula amewataka wananchi wa wilaya ya Iramba kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa wahamiaji haramu ili kuthibiti raia wa kigeni na yeyote atayebainika kuficha wahamiaji haramu kwenye eneo lake atachukuliwa hatua kali za kisheria. Alitoa wito kwa wananchi kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka watoe taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogudua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao

Diwana wa kata ya Kinampanda Mhe: Justus Makala (CCM) akiongea na wananchi wa Kisharita.


Announcements

  • TANGAZO KUHUSU UJIO WA MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA WILAYA YA IRAMBA-KIOMBOI February 20, 2026
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 02, 2026
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • View All

Latest News

  • MAONESHO YA MATUMIZI YA PEMBEJEO ZA KILIMO (MBEGU, MBOLEA NA VIUATILIFU) HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA DISEMBA 29-30, 2025

    December 28, 2025
  • HERI YA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2026

    December 25, 2025
  • DC MWENDA AWATAKA WALIMU IRAMBA KUONGEZA UBUNIFU NA BIDII KUINUA UFAULU

    December 09, 2025
  • HERI YA MIAKA 64 YA UHURU WA TANZANIA BARA

    December 09, 2025
  • View All

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
More Videos

Quick Links

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Related Links

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    KIOMBOI, IRAMBA

    Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Telephone: 026 - 2532253

    Mobile: 026 - 2533001

    Email: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.