Wanachama wa CCM na wananchi wa wilaya ya Iramba wakimusikilza Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, katika ziara ya kutembelea wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Viongozi mbalimbali wakimuskiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, katika ziara ya kutembelea wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, akiwa kwenye na wakinamama katika ziara ya kutembelea wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula, Mbunge wa jimbo la Iramba mashariki Mhe: Dkt Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iramba Mhe: Samwel Ashery Joel na Diwani wa Kata ya Shelui wakiwa kwenye picha ya pamoja ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, katika ziara ya kutembelea wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iramba Mhe: Samwel Ashery Joel akizungumza na wananchi kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mbuge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe, akisalimia wananchi wa wilaya ya Iramba kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo,
wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mhe:Dkt Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa wilaya ya Iramba katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mhe: Hassan Kilimba akizungumza na wananchi wa Iramba katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo wilayani Iramba mkoani Singida.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo akizungumza na wananchi katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mhe: Rodrick Mpogolo, amefanya ziara ya kutembelea wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mhe Mpogolo amekutana na wananchi wa Iramba akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mhe: Hassan Kilimba, mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mhe: Dkt Mwigulu Nchemba, Mhe Asyrose Mattembe mbunge viti maalum (CCM) viongozi mbalimbali wa mkoa wa singida na viongozi wa wilaya ya Iramba.
Mhe: Mpogolo akizungumza na wananchi amesema “Nawashukuru sana kwa Mapokezi makubwa, nimefurahi sana, nawashukuru sana kwa moyo wenu wa dhati Mwenyekiti wa CCM wilaya, Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wote, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba na watendaji nawashukuru kwa kazi mnazozifanya kwa ajili ya kuwaletea wananchi wa Iramba maendeleo alisema Mhe: Mpogolo
Aliongeza kusema “Mhe: Rais Dkt, John Pombe Joseph Magufuli anawasalimu sana wananchi wa Iramba, Rais anawapenda wananchi wa Iramba pamoja na watanzainia wanyonge kama sisi, serikali yenu ipo kwa kutatua changamoto za wananchi alisema Mhe: Mpogolo
Tanzania inasonga mbele kwa kasi kubwa sana, Watanzania tunabahati kwa sababu Mhe: Rais anawapenda watanzania naomba tumuunge mkono kwa dhati kabisa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa nchi yetu, anafanya mambo makubwa sana Watanzania tunajivunia sana na Rais wetu, aliongeza kusema Mhe: Mpogolo
Amewambia Watendaji waendelee kuchapa kazi na wahakikishe miradi yote inayotekelezwa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii ziwe na viwango vinavyoridhisha, “miradi ya kijamii itekelezwe katika kiwango bora, inasaidia kupunguza gharama zisizokuwa za lazima na kuwawezesha wananchi kupata kwa wakati mahitaji muhimu ya kijamii.
Mhe: Mpogolo amewaasa viongozi mbalimbali na wananchi wa Iramba kuheshimiana na kuwa na mshikamano kwa ajili ya kujenga nchi yetu kwa pamoja, “Shariti la kwanza la katiba ya CCM lazima kuheshimu watu, Viongozi wa CCM tunapaswa kuwaheshimu waliokuchagua, lazima kwenye chama tuwe na heshima, tuheshimu wananchi wetu. Tunahitaji CCM yenye mshikamano ili tuwahudumie wananchi wetu na kuwaletea maendeleo. Binadamu wote ni sawa, kila mmoja anastahili heshima na kutambuliwa utu wake. lazima mshirikiane kwa pamoja ili tuweze kuleta maendeleo ya kweli. Tunaenda kufanya uchanguzi wa serikali za mitaa, na Kuboresha daftari la tume ya taifa la wapiga kura, tushirikiane Kutambua vijana wote ambao wanasifa za mpiga kura, wote waandikishwe alisistiza Mhe: Mpogolo
Mbunge wa Iramba Magharibi Mhe: Dkt Mwigulu Nchemba ametoa pongezi za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa vituo vya Afya vya Ndago na Kinampanda, kuleta umeme, ujenzi wa madaraja, maji, ujenzi wa mabweni na miradi mingi katika wilaya ya Iramba. “Namshukuru sana Rais Magufuli kwa Ujenzi wa vituo vya afya vya Ndago na Kinampanda, sisi huku hatuiti vituo vya afya bali tunaviita hospitali, Ujenzi wa madaraja, kutuletea umeme, ujenzi wa mabweni kwa ajili wa wanafunzi wetu, uchimbaji na usambazaji wa Maji na miradi mingi alisema Dkt. Nchemba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.