• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Lemomo Kiruswa amempa wiki moja Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda kutatua mgogoro

Posted on: January 18th, 2022

Na Hemedi Munga

tehama@irambadc.go.tz

Singida - Iramba. Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Lemomo Kiruswa amempa wiki moja Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda kwa kushirikiana na Kaimu Afisa Madini mkoa wa Singida kutatua mgogoro wa duara namba 22 kati ya wanaodaiwa kuwa wawekezaji na wanachama wa duara hilo.

Dkt. Kiruswa ametoa agizo hilo leo Jumanne Januari 18, 2022 wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha na kusikiliza kero katika kijiji cha Nkonkilangi wilayani hapa.

“Ninakuagiza Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Kaimu Afisa Madini Singida kutatua mgogoro huu na ifikapo tarehe 30 januari tupate taarifa kuwa hapa hakuna mgogoro.” Aliagiza Naibu waziri huyo na kuongeza kuwa

“Kati ya vitu ambavyo hatuitaji kuviona katika hii sekta ni migogoro tunahitaji kuielea hii sekta kwa kuhakikisha hakuna migogoro ili wachimbaji wanufaike na ikitokea kuna mgogoro sumbufu unaosababisha wachimbaji kutopata rasilimali hii tutaifuta hiyo leseni.”

Amewahakikishia wachimbaji hao kuwa serikali inahitaji kuona kuwa kila mmoja anapata haki yake na katu serikali haitaji kuona wachimbaji wanagombana.

Akiongelea kuhusu maombi ya namna bora kuwasaidia kutoa maji yanayodaiwa kuwa ni kero kubwa inayosababisha wachimbaji kutumia gharama kubwa na kutopata manufaa kwa sababu ya maji, alisema kuwa wanahitaji kuainisha mahitaji yote ya vifaa hivyo na kuviweka katika mkakati wa serikali kwa ajili ya kuvipata ili kusaidia kutatua changamoto hiyo.

Halikadhalika, amewaahidi wachimbaji hao kutuma timu ya wataalamu kutoka wizarani itakayowasaidia wachimbaji kubaini miamba sahihi ya kuchimba ili kupata madini kwa wepesi.

Akiongea katika eneo hilo la mgodi mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda alisema kuwa wachimbaji wadogo hao katika mwaka wa fedha 2020/2021 wemeweza kuuza gramu 319,000 katika soko la madini Shelui  na kuweza kuingizia serikali kiasi cha Tsh 37 bilioni.

Aidha ametumia nafasi hiyo kumuomba Naibu waziri huyo kuwasaidia wachimbaji hao kupata vifaa vitakavyowasaidia kuondoa maji ili waweze kuchimba dhahabu kwa njia nyepesi.

Akijibu hoja za wachimbaji Kaimu Afisa madini mkoa wa Singida, Chone Malembo amewataka wachimbaji hao, kero walizonazo wakae kuzizungumzia ili wazitatue kwa sababu hakuna kinachoshindikana katika mazungumzo.

Malembo alibainisha sifa za kupata leseni kwa mujibu wa kifungu cha nane cha sheria ya madini kuwa ni mtua kuwa mtanzania mwenye umri usiokuwa chini ya miaka 18, hajawahi kushitakiwa na kutangazwa na mahakama kama aliyekosa, tini namba, picha mbili za paspoti  na kitambulisho aidha cha udereva, kura au cha taifa.

Kwa upande wake mmoja wa wachimbaji katika duara hilo namba 22, Zahara Abdilahi alisema kuwa kwa nini wao kama viongozi wa Ushirika wa Ukombozi hawachukui asilimia ya ofisi, hivyo anaomba leo hilo lipatiwe ufumbuzi.

Naye Samora Omari anayedaiwa kuwa mwekezaji wa duara namba 22 kuhoji kuwa ninani anastahiki kuwa na leseni ya kuchimba madini kwa kuzingatia sheria za nchi ya Tanzania.

MWISHO

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • KIDATO CHA KWANZA KURIPOTI SHULE January 13, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"

    March 24, 2025
  • DC MWENDA AWASISITIZA WALIPA KODI KUFANYA MAKADIRIO YA KODI KABLA YA MACHI 31, 2025

    March 20, 2025
  • DC MWENDA NA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA WACHANGIA JUMLA YA MADAWATI 98 SHULE YA MSINGI MSANSAO ILIYOPO KATA YA MTEKENTE

    March 10, 2025
  • WALIMU WAKUU 108 WA SHULE ZA MSINGI NA MAAFISA ELIMU KATA 20 WILAYANI IRAMBA WAPEWA MAFUNZO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI FANISI KUPITIA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA ZA WALIMU WAKUU NA MAAFISA ELIMU KATA

    March 19, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.