• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Serikali ya mkoa wa Singida yatambulisha rasmi soko la madini

Posted on: May 3rd, 2019

SERIKALI YA MKOA WA SINGIDA YATAMBULISHA RASMI SOKO LA MADINI

Serikali mkoani Singida imetekeleza kwa kishindo agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, la mikoa yenye madini kuanzisha soko ndani ya siku 7 alizotoa, kwa kushuhudia uuzaji na ununuzi rasmi wa dhahabu ndani ya soko hilo la dhahabu katika mkoa wa Singida.

Akizungumza jana 01 Mei, 2019 akiwa katika soko hilo la madini mkoani Singida mara baada ya kukagua shughuli zitakazofanyika ndani ya soko hilo, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema, soko hilo litabadili uchumi wa mkoa wa Singida.

“Soko hili litabadili kabisa sio uchumi tuu wa dhahabu lakini pia uchumi wa Singida, na hii itadhihilisha usemi unaosemwa kuwa Singida ni njema tena ni njema sana” Dkt. Nchimbi.

Amesema, Serikali ya mkoa wa Singida ipo tayari, inauwezo na imejiandaa kikamilifu kushiriki na kutimiza haki na wajibu wake wa kuhakikisha soko hilo linakuwa endelevu na lenye heshima kubwa nchini.

Akisisitiza zaida amesema, wadau wote wanaotakiwa kuwepo kwenye mnyororo wa biashara ya madini ya dhahabu ndani ya soko hilo wapo tayari, wakiwemo wauzaji, wanunuzi, taasisi za kifedha (benki), Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, pamoja na vyombo vyote vinavyohusika.

“Kwahiyo hapa ndipo penyewe na pamekamilika, muuzaji au mnunuzaji ataingia hapa atatoka hana fedha lakini fedha zake zitakuwa kwenye mfumo wa kibenki” Dkt. Nchimbi.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa wa Singida amewashukuru wachimbaji pamoja na wauzaji wa dhahabu mkoa wa Singida kwa ushirikiano walioutoa kwa Serikali ya mkoa katika kufanikisha kukamilika kwa soko hilo la madini mkoa wa Singida.

“SOKO LA DHAHABU KIMKOA NI HILI HAPA”

“Na wote wanaohusika na dhahabu wapo tayari kuuza dhahabu hapa, na wakati wote tuwe pamoja kuwawezesha ndugu zetu hawa ili waweze kulitumia soko hili vizuri zaidi” Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa wakurugenzi, watendaji pamoja na watumishi wote mkoani Singida kwa kulitangaza soko hilo kwa wahusika wote ili wajue kuwa soko la dhahabau lipo ndani ya mkoa wa Singida.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, ametoa rai kwa wachimbaji wadogo mkoani Singida kutumia fursa hiyo ya upatikanaji wa soko la madini ndani ya mkoa ili kuinua uchumi wao na kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, mkoa na taifa kwa ujumla.

“Leo tunaona juhudi za mheshimiwa mkuu wetu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi za kuhakikisha kwamba tunapata hili soko la madini”

“Nitoe rai kwa wachimbaji wadogo kwamba hii ni fursa na fursa hii lazima tuitumie vizuri, fursa hii ndio itakayotutoa hapa tulipo kwenda sehemu nyingine zaidi kiuchumi. Na huko tunako elekea tunahitaji kuelekea mahali ambapo mkoa huu wa Singida ndio utakaokuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania” Mhe. Sima

Nao, Wachimba wa madini mkoa wa Singida wameishukuru Serikali kwa ujio wa soko hilo la madini mkoani Singida kwani, kupitia soko hilo litapelekea ulipaji sahihi wa kodi za Serikali chini ya usimamizi makini wa Serikali ya Awamu ya Tano tofauti na hapo awali. 

Aidha, wamempongeza Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida kwa kuliweka soko hilo mahali salama na panapostahili.

“Ujio wa soko hili kwetu sisi wachimbaji imekuwa ni muhimu sana kwa sababu tumepata sehemu ya uhakika na mizani iliyohakikiwa” Amesema, Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini mkoa wa Singida.

Naye, Makamu mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo mkoa wa Singida amesema, walikuwa na hamu kubwa sana ya kuwa na soko la madini ndani ya mkoa ili kuondokana na adha waliyokuwa wanaipata hapo awali ya kutokuwa na mahali salama pa kufanyia biashara hiyo ya madini.

“Kitendo kilichofanyika leo cha kushuhudia rasmi uuzaji na ununuzi wa dhahabu ndani ya soko jipya mkoani Singida, kinatupa sisi wachimbaji wadogo mwanga wa kuanza kuleta dhahabu ili kuuziwa hapa ili kukuza uchumi wa mkoa na taifa letu”.

“Tunaahidi dhahabu zote zinazopatikana ndani ya mkoa wetu wa Singida zitauzwa hapa, na wachimbaji wetu wapo tayari kuuza hapa, hivyo hakutakuwa na utoroshwaji wa dhahabu tena.” Amesema, Makamu mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo mkoa wa Singida.

Wamesema, awali palikuwa na utaratibu mbaya katika biashara ya dhahabu. Kuitoa mkoani Singida kupeleka mikoa mingine iliyokuwa ikisababisha wafanyabiashara hao wa madini kutumia njia zilizokuwa kinyume cha sheria na taratibu, lakini sasa wachimbaji wamefurahi sana kwa kuwa na soko la madini ndani ya mkoa wa Singida. 

MATUKIO KATIKA PICHA

 Kaimu Afisa Madini mkoa wa Singida Bw. Chone Lugangizya Malembo (kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya mkoa wa Singida waliojitokeza kushuhudia uuzwaji na ununuzi wa dhahabu rasmi ndani ya soko la madini mkoani Singida.


PICHA YA PAMOJA

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • KIDATO CHA KWANZA KURIPOTI SHULE January 13, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"

    March 24, 2025
  • DC MWENDA AWASISITIZA WALIPA KODI KUFANYA MAKADIRIO YA KODI KABLA YA MACHI 31, 2025

    March 20, 2025
  • DC MWENDA NA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA WACHANGIA JUMLA YA MADAWATI 98 SHULE YA MSINGI MSANSAO ILIYOPO KATA YA MTEKENTE

    March 10, 2025
  • WALIMU WAKUU 108 WA SHULE ZA MSINGI NA MAAFISA ELIMU KATA 20 WILAYANI IRAMBA WAPEWA MAFUNZO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI FANISI KUPITIA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA ZA WALIMU WAKUU NA MAAFISA ELIMU KATA

    March 19, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.