• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Comments |
Iramba District Council
Iramba District Council

The United Republic of Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Iramba District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

SERUKAMBA APIGA MARUFUKU KUCHUNGIA MIFUGO HIFADHI YA MISITU YA SEKENKE

Posted on: May 2nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amepiga marufuku shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima, kuchungia mifugo na kuanzisha ujenzi wa makazi katika hifadhi ya Msitu wa Sekenke uliopo Wilaya ya Iramba ili kulinda msitu huo utakaosaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

RC Serukamba amesema hayo leo Mei 2, 2023 wakati akisikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Masagi kata ya Mtoa Wilayani Iramba ambapo wananchi waliiomba serikali ya Wilaya kuwaruhusu kuchungia mifugo yao kwenye Hifadhi ya Msitu huu.

Mkuu huyo amesema kuwa shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi za misitu ndio sababu ya kupelekea ukame ambao umekuwa ukiathiri shughuli za uzalishaji kama vile kilimo hivyo amewataka wananchi hao kuanza kutenga Maeneo ya malisho pamoja na kuanzisha kilimo cha Nyasi kwaajili ya Kulisha Mifugo yao.

“Wazee nyie mmekuwa hapa kote huko kulikuwa na misitu kwasababu wazazi wetu waliinda misitu haiwezekani sisi tuache kulinda misitu Mlima Sekenke lazima tuulinde, Habari ya kuchunga, Kukata kuni huko haipo, umefika wakati mtu awe anatenga eneo la kufugia na ardhi ambayo utalima, tubadilike muanze kuwa na maeneo ambayo mtakuwa mnalima nyasi za kulisha mifungu sasa hivi Dunia Imefikia huko” Alisema RC Serukamba

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Yusuph Mwenda amesema kuwa kuharibiwa kwa misitu katika kata ya Mtoa na Maeneo mengine kumepelekea kuharibu vyanzo vya maji na mvua hali ambayo imeathiri uzalishaji ukilinganisha na hapo awali ambapo kulikuwa na misitu mingi ambayo ilikuwa inavutia mvua.

DC Mwenda Aliongeza kuwa awali Wilaya ya Iramba ndio ilikuwa eneo pekee lenye vyanzo vingi vya maji kwa kuwa na Maziwa na mabwawa ikiwemo ziwa Kitangiri, Doromoni, Mabwawa ya Urughu na Mayanzani lakini kwa sasa kutokana na uharibifu wa misitu vyanzo hivyo vimeathirika na vingine kukauka.

Kero Nyingine iliyowasilishwa na wananchi wa Masagi ni katika idara ya afya ambapo wananchi wa Kijiji hicho walimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa wahudumu wa afya wamekuwa hawatoi huduma nzuri kwa wananchi hasa akina mama wakati wa kujifungua na kupelekea kujifungulia nyumbani.

Kufuatia Kero hiyo RC Serukamba amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuanza kuwafuatia wataalam na wahudumu wa afya ngazi za Chini ili kuhakikisha huduma nzuri zinatolewa kwa wananchi.

Pamoja na Mambo mengine Rc Serukamba amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba kumalizia hatua zilizo bakia kwenye Zahanati ya Kijiji cha Masagi ambapo ametoa siku tano zahanati hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Announcements

  • TANGAZO KUHUSU UJIO WA MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA WILAYA YA IRAMBA-KIOMBOI February 20, 2026
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 02, 2026
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • View All

Latest News

  • MAONESHO YA MATUMIZI YA PEMBEJEO ZA KILIMO (MBEGU, MBOLEA NA VIUATILIFU) HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA DISEMBA 29-30, 2025

    December 28, 2025
  • HERI YA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2026

    December 25, 2025
  • DC MWENDA AWATAKA WALIMU IRAMBA KUONGEZA UBUNIFU NA BIDII KUINUA UFAULU

    December 09, 2025
  • HERI YA MIAKA 64 YA UHURU WA TANZANIA BARA

    December 09, 2025
  • View All

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
More Videos

Quick Links

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Related Links

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    KIOMBOI, IRAMBA

    Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Telephone: 026 - 2532253

    Mobile: 026 - 2533001

    Email: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.