SHILINGI MILIONI 99 ZIMETUMIKA KUKAMILISHA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASAGI KILICHOPO KATA YA MTOA, TARAFA YA SHELUI WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda; Amezindua rasmi Zahanati ya Kijiji cha Masagi Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Zahanati ambayo inakusudiwa kuhudumia wananchi wapatao 3,117 katika Kijiji hicho Cha Masagi.
Aidha DC Mwenda,Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi, kwa lengo la kushuhudia uzinduzi wa Zahanati hiyo amewataka wananchi hao kuhudhuria kikamilifu na Kupata matibabu katika Zahanati hiyo, kwani kwa sasa changamoto ya kufuata matibabu kwa mwendo mrefu umeisha.
Mwenda Amesema kuzinduliwa kwa Zahanati hiyo kutaondoa kabisa vifo vya akina Mama na watoto ambao walikuwa wanayapata wakati wanafuata Matibabu Shelui au Mtoa na halikadhalika katika Hospitali ya Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya, Amesema kwa sasa vifo vya akina mama vitapungua kwa asilimia kubwa kutokana na kukamilika kwa Zahanati nyingi katika vijiji Wilayani Iramba, lakini pia pindi vituo vya Afya vya Mtoa, na Shelui vitakapokamilika vitafanya vifo vya mama na mtoto kuwa ni historia katika nchi.
Aidha Mwenda amebainisha kuwa Mpaka sasa,Tayari Tsh. Milioni 280 zimeletwa kumalizia Kituo cha Afya Mtoa, Huku jumla ya Tsh.Milioni 120 zimeingia tayari kwa ajili ya Kukamilisha Kituo Cha Afya Shelui, na kuongeza kuwa tayari shilingi Milioni 200 zimeletwa Kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kinambeu Ili kuhudumia wananchi wa eneo hilo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dkt. Hussein Sepoko amesema Zahanati ya Masagi imekamilika na tayari imepewa Vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 24 huku wahudumu wa Afya wawili tayari wamefika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Aidha wananchi wa Kijiji hicho wameishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali kuhusiana na Afya zao na sasa wamepona kilio chao cha muda mrefu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.