Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu kuunda Vikundi kwa ajili ya kuanzisha biashara kwa lengo la kipatiwa Mikopo ya Asilimia 10 ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Mwenda ameyasema hayo wakati Alipofanya ziara kwenye Vijiji vya Kata ya Kidaru,akijibu swali lililoulizwa na Anderson Naligia kutoka Kijiji cha Kidaru akitaka kujua ni lini Serikali iawaajiri Vijana wao kwani wamewasomesha kwa kuuza mifugo yao na bado hawajaajiriwa wapo mtaani.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imejipanga kutenga zaidi ya Milioni 348,969,986.25 ili kuwawezesha Wananchi katika kujikwamua kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo inayotoka na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya yetu.
“Tuna Vijana zaidi ya 25000 Wilayani Iramba,Serikali inaendelea kutoa ajira,niwaombe tuwafundidhe Vijana watengeneze Vikundi kwa ajili ya kupatiwa Mikopo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali wanazozifanya katika maeneo yao” Amesema DC Mwenda
Aidha Mwenda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 toka alipositisha mikopo hii mwezi wa nne mwaka 2023.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.