• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO UTAONGEZA TIJA YA UZALISHAJI WA MAZAO NCHINI-DC MWENDA

Posted on: November 4th, 2024

Zoezi la upimaji wa afya ya udongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwemo chakula, biashara pamoja na mazao ya bustani.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda alipokutana na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo, Eng. Juma Omary Mdeke pamoja na wadau wa kilimo kutoka shirika la Helvetas kwenye Mradi wa UKIJANI wakati wa ufuatiliaji wa zoezi la upimaji wa afya ya udongo linaloendela Wilayani humo kuanzia tarehe 4 Novemba 2024.

“Zoezi hili la upimaji wa afya udongo litatusaidia kutambua aina ya udongo, mazao yapi yanafaa kulimwa katika eneo husika na kupata matumizi sahihi ya mbolea,” amesema Mhe. Mwenda.

Naye Eng. Juma Omary Mdeke amesema zoezi hilo litahusisha vijiji 78 katika Halmashauri hiyo na kuchukua Sampuli zisizopungua 400 kwa ajili ya uchakataji na kupata matokeo sahihi na kuwaelimisha wakulima namna gani ya kulima ili kufikia malengo ya Serikali kupitia Agenda 10/30.



Aidha, kwa upande wake Meneja wa Mradi wa UKIJANI kutoka shirika la Helvetas Mkoani Singida, Bi. Shoma Nangale ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa mpango huo madhubuti wa upimaji wa afya ya udongo ambao utasadia kukuza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kuwa Udongo ndio chanzo cha kilimo.

Baada ya Kukamilisha ufuatiliaji wa zoezi hilo la upimaji wa afya ya udongo Wilayanii Iramba, Eng. Mdeke aliambata na Meneja wa Mradi wa UKIJANI, Bi. Shoma Nangale kutoka Shirika la Helvetas kutembelea maeneo mbalimbali ya wanufaika wa mradi huo katika wilaya ya Ikungi pamoja na Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida tarehe 4-5 Novemba, 2024.

Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi ya kilimo kwa kutekeleza zoezi la kutambua na kupima afya ya udongo kwa nchi nzima ili kuandaa ramani ya udongo nchi nzima itakayo onesha hali ya udongo ili kuongeza tija na uzalishaji ili kufikia lengo la kukuza Sekta ya Kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.



Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI June 05, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • DC MWENDA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA AMALI KITUKUTU

    May 08, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    May 06, 2025
  • DC MWENDA ATOA WITO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUIMARISHA UFUNDISHAJI KWA MADARASA YA MITIHANI

    May 06, 2025
  • JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WILAYANI IRAMBA LATOA ELIMU YA KINGA DHIDI MAJANGA YA MOTO KWA MADIWANI NA WANANCHI

    May 02, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.