Hemedi Munga Irambadc
Iramba. Waziri wa Katiba na Sheria, Frofesa Palamagamba Kabudi amewataka vijana wote Nchini kuona fahari ya kuzaliwa Tanzania.
Kabudi ametoa wito huo leo Jumanne Agosti 4, 2021 wakati akiongea na watumishi wa kada tofauti wilayani Iramba Mkoa wa Singida katika ukumbi Mkubwa wa Halmashuri hiyo alipofanya ziara yake mjini hapo.
Akiongea na watumishi hao, Waziri Kabudi amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya Nchi chache Barani Afrika na Duniani kwa ujumla iliyofanikiwa kujenga utaifa.
“Watumishi wenzangu fahamuni kuwa Tanzania na hasa vijana muone fahari mmezaliwa watanzania na leo hamjazaliwa na makabila yenu, muwe na fahari kwani Tanzania ni Taifa ambalo limejiwekea misingi inayojali watu wote” amesema Prof. Kabudi nakuongeza kuwa
“Sisi ni Taifa, la uchumi wa kati, lililopita katika misukosuko na dhuruba lakini limebaki kuwa imara na linasonga mbele chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan.”
Akieleza lengo la ziara yake Wilayani hapo kuwa ni kuona utendaji wa haki, demokrasia, utawala bora na utawalaya wa sheria kwa namna ambavyo vilieelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) vinatekelezwa kwa sababu ndio chama kinachoisimamia Serikali.
Aidha amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo, Suleiman Mwenda kuwa yeye ni mahiri na kuwa ataweza kuingoza Wilaya hiyo kupitia Ilani ya Chama.
Awali akiwasilisha hali ya utendaji wa haki, utawala bora na utawala wa sheria katika wilaya hiyo mbele ya Waziri huyo, Mkuu huyo wa Wilaya, Suleiman Mwenda amesema kuwa Wilaya imeendelea kutekeleza shughuli zake kwa kufuata misingi ya utawala bora kwa kuhakikisha kunakuwepo uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji, utawala wa sheria na majadiliano.
Mwenda amefafanua kuwa Wilaya imefanikiwa kuhakikisha inawajibika ili wananchi wapate huduma za msingi kwa wakati na kiwango kinachotakiwa.
Aidha amebainisha kuwa serikali ya wilaya imefanikwa kuendesha shughuli zake kwa uwazi na kufanikiwa kuwapa fursa wananchi kupata taarifa zote muhimi zinazohusu mipango na makusanyo ya fedha na matumizi yake yanabandikwa katika mbao za matangazo, hivyo kuwapa fursa wananchi kujuwa nini kinaendelea katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ibrahim Mjanaheri amemshukuru Waziri huyo kwa namna walivyorekebisha sheria ya madini na kuhakikisha rasilimali za Nchi zinabaki kuwanufaisha watanzania.
Pia amemuomba kutoa kipaumbele cha ujezi wa Mahakama ya Wilaya ya kisasa ijengwe Wilayani hapo kwa sababu itasaidia kutoa taswira nzuri ya wilaya.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi anayeshughulikia Wilaya ya Iramba na Mkalama, Christopher Makwaya ameseama kuwa Mahakama imekuwa na spidi ya kuendesha mashauri kwa njia ya kidigitali.
Makwaya amesema kuwa hali hiyo inasaidia kupata nakala ya hukumu punde tu baada ya shauri la mtuhumiwa kukamilika na kufanikiwa kusogeza huduma kwa wananchi.
MWISHO
Waziri wa Katiba na Sheria, Frofesa Palamagamba Kabudi katikati akiwa katika picha na ya pamoja na baadhi ya viongozi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya iramba, Suleiman Mwenda na Kulia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ibrahim Mjanaheri. Picha na Sarapion Kakiziba
Viongozi mbalimbali wakifuatilia nasaha za Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Sarapion Kakiziba
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.