• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

ZAIDI YA BILIONI 10 KUBORESHA SKIMU YA UMWAGILIAJI MASIMBA, IRAMBA, SINGIDA.

Posted on: November 22nd, 2024

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Masimba katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, wenye thamani ya shilingi bilioni 10.5.


Mradi huo, unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, unalenga kuongeza tija ya kilimo kwa wakulima wa eneo hilo na kuboresha maisha ya zaidi ya watu 24,000 kutoka vijiji vya Masimba, Urughu, Mlandala, Mang’ole, na Ujungu.


Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi eneo la mradi kwa mkandarasi iliyofanyika katika Kata ya Urughu, Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba, alisisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Kilimo, chini ya uongozi wa Waziri Hussein Bashe, zinaimarisha kilimo cha kisasa na kuleta mapinduzi katika sekta hiyo, ambayo ni mhimili wa uchumi wa wananchi wengi nchini.


Dkt. Nchemba, aliongeza kuwa mradi huo ni mfano wa jinsi serikali inavyotekeleza dira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya kilimo, na hasa kilimo cha umwagiliaji, ili kuhakikisha uzalishaji endelevu na maendeleo ya jamii za vijijini.


Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Miundombinu, Ndugu. Raphael Laizer, alifafanua vipengele vya mradi, ambavyo ni pamoja na: Ukarabati wa bwawa na sehemu ya utoro wa maji, Kuondoa mchanga na tope ndani ya bwawa ili kuongeza ujazo wake kwa mita za ujazo 250,000, Ujenzi wa mfereji mkuu wa mita 200 kwa kiwango cha zege, Ujenzi wa mifereji ya upili yenye urefu wa mita 9,254 kwa kiwango cha zege.


Nae Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Mwenda, alisema mradi huu ni hatua kubwa inayojibu kilio cha muda mrefu cha wakulima wa eneo hilo kwa kutatua changamoto za upatikanaji wa maji ya uhakika kwa kilimo.


Skimu hiyo itakuwa na eneo la ekari 1,800 za umwagiliaji, ambapo wakulima watazalisha mazao ya mpunga na mbogamboga kwa wingi, hatua inayotarajiwa kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha.



Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI June 05, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • DC MWENDA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA AMALI KITUKUTU

    May 08, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    May 06, 2025
  • DC MWENDA ATOA WITO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUIMARISHA UFUNDISHAJI KWA MADARASA YA MITIHANI

    May 06, 2025
  • JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WILAYANI IRAMBA LATOA ELIMU YA KINGA DHIDI MAJANGA YA MOTO KWA MADIWANI NA WANANCHI

    May 02, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.