Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Iramba Mheshimiwa Innocent Msengi Oktoba 21,2024, imefanya ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo ya miundombinu ya elimu na afya katika wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo Wajumbe hao waliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Lengo la ziara hiyo likiwa ni kutathmini maendeleo ya miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaokubalika.
Wakati wa ziara hiyo, kamati ilikagua miradi mbalimbali ya Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari inayojengwa Kata ya Mtoa kupitia Sequip kwa gharama ya Milioni 544,225,626.00, Ujenzi wa Mabweni 2,Vyumba vya madarasa 4,matundu 12 ya Vyoo vya wanafunzi kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha Tano Shule ya Sekondari Kinambeu ujenzi wa vyumba vya madarasa vitano na matundu Sita ya Vyoo Shule ya Msingi Tyeme kwa gharama ya Mil.126,200,000, na Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Shule ya Sekondari Iramba (2 in 1) kwa gharama ya shilingi Milioni 95,000,000
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Innocent Msengi amewapongeza Wataalamu wa Halmashauri na wasimamizi wa Miradi kuhakikisha Miradi inatekelezwa kwa ubora ili iweje kudumu muda mrefu na kutoka huduma Bora kwa wananchi.
"Tumefurahishwa na maendeleo ya miradi hii," alisema Mhe. Innocent Msengi. "Tunawaagiza wasimamizi wa miradi hii wahakikishe inakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Tunataka wananchi wa Iramba waanze kunufaika na miradi hii haraka iwezekanavyo,Pia Wataalamu hakikisheni mnawapa msaada Watumishi wote wenye Miradi juu ya changamoto wanazokutana nazo kwenye mfumo wa manunuzi wa NEST ."Alisema Mheshimiwa Msengi.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango pia walipongeza mwenendo wa ujenzi wa miradi hiyo na kuwataka wasimamizi wahakikishe kuwa inajengwa kwa uadilifu na kwa uwazi. Walisisitiza pia umuhimu wa ushirikiano kati ya kamati za ujenzi na wananchi katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa mafanikio.
Aidha ziara hii ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ya kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa uwazi. Halmashauri inaamini kuwa miradi hii itaboresha maisha ya wananchi wa Iramba kwa kiasi kikubwa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.