Kampuni ya EACOP imeanza usajili na mafunzo ya online kwa wiki 8 yatakayofwatiwa na mtihani wiki ya 9 kwa ajili ya kupata vijana 140 wenye umri kati ya miaka 18-28 watakaoshiriki katika mlolongo wa mafunzo yenye nia ya kupata wafanyakazi watakaoajiriwa wakati wa uendeshaji (operation & maintenance) wa miundombinu ya bomba la mafuta .
Vijana hao 140 watahudhuria mafunzo kwa miezi 3 VETA Moshi, Miezi 3 Arusha Technical College, Miezi 6 UPIC - Uganda, Miezi 4 abroad.
Kila hatua utatakiwa kufaulu ili kuendelea hatua inayofuata.
Usaili na ushiriki wa mafunzo ya online unalenga kuanzia wahitimu wa kidato cha nne, cha sita vyuo vya ufundi na vyuo vikuu.
Washiriki wa kike na wale wanaotokea mikoa inayopitiwa na mradi wanahimizwa kujitokeza ili wachukue fursa hii ya kipekee
Usajili na module ya kwanza unaanza kesho tarehe 5th June mpaka 25th June, 2023 kupitia link
Angalizo Dirisha la usaili likifungwa hautapata nafasi ya kujisaili kwa hiyo wahi hii fursa sasa ivi..
Kwa maelezo zaidi pitia tovuto https://eacop.com/mooc-tanzania/
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.