Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda, amepongeza walimu na wanafunzi wa Wilaya ya Iramba kwa kufanya vizuri katika Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2025.
Amesema matokeo hayo yanaonyesha kwa namna ya pekee juhudi, nidhamu na ari ya kujifunza iliyojengwa kwa wanafunzi, sambamba na uongozi makini wa walimu katika kusimamia taaluma. Mheshimiwa Mwenda amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya walimu, wazazi na Serikali umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha maendeleo ya elimu wilayani humo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya, kiwango cha ufaulu kimeongezeka na kufikia asilimia 79.6, ongezeko la asilimia 2.3 kutoka asilimia 77.3 mwaka 2024. Ameeleza kuwa ongezeko hilo ni ishara ya mwelekeo chanya unaoendelea kujengwa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Amehitimisha kwa kuwasihi walimu na wanafunzi kuendeleza bidii hiyo ili Iramba izidi kuwa mfano wa mafanikio katika elimu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.