Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Afisa TEHAMA wa Mkoa wa Singida, Baraka Emmanuel amewaomba Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali kutumia taarifa zinazopatikana katika mifumo ya TEHAMA kupanga mipango na kufanya maamuzi yanayolenga kuinufaisha Halmashauri.
Emmanuel ameyasema hayo leo Alhamisi februari 20, 2020 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara na Vitengo (CMT) yaliofanyika Ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mjina hapa.
Mafunzo hayo yamekusudia kujenga uwelewa na uwazi kwa Wakuu hao kuelewa matumizi ya mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayotumika katika Mamlaka za serikali za Mitaa.
Kupitia mifumo hiyo imeweza kurahisisha uandaaji wa taarifa na utendaji wa kazi mbalimbali katika kupanga na kuamua huku wakizingatia vipaumbele vilivyotokana na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo.
Amesema kua Wakuu wa Idara na Vitengo wanapaswa kuifahamu mifumo ili kujua taarifa zinazopatikana na kuweza kuzichambua kwa lengo la kupanga makisio ya wilaya yao (projection).
Aidha amewashauri Wakuu hao kua na tabia ya kutoa zawadi kwa Idara iliyofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vilivyoko chini ya Idara hiyo.
“ Mnapaswa kufahamu mchango wa kila Idara ukoje na kuandaa zawadi kuzipatia Idara zinazochangia mapato zaidi,” alishauri Emmanuel
Akichangia mada Afisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Ndugu Sanga amewaomba Wakuu hao kua na ushirikiano hasa kwa wale wanaokuja kukata leseni, kuhakikisha wanalipa na kodi ya huduma (service levy).
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo, B’hango Lyangwa amemuhakikishia Afisa huyo kua mafunzo waliyoyapata watayafikisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri hiyo kwa hatua zaidi.
Lyangwa amewaomba Wakuu wa Idara na Vitengo kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato.
“Tunapaswa kuweka kipaumbele kuimarisha ukusanyaji wa mapato kulingana na tathimini zilizotolewa,” amesisitiza
Kua na tabia yakuweka nguvu kubwa kwenye kukusanya mapato na si kuweka nguvu kubwa kwenye matumizi na kujihisi kua wewe sio sehemu ya wanaotakiwa kukusanya mapato.
Katika mafuzo hayo mifumo ifuatayo imefumdishwa, LGRCIS, GoTHOMIS, FFARS, PLANREP, iMIS, TANEPS, PMIS, GMS, PSSN, MIS, Prem, Prems, BEMIS, HeMIS, GSPP, EPICOR.
GWF, eLMS, DHI , HRHIS, Tool ya WISN+POA, DCMS, Mfumo wa sense ya WALIMU, Mfumo wa SELFORM, TSM 9 Mtandao, HELP DESK SUPPORT – TAMISEMI na eGa
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.