By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewaagiza wananchi kwenda kuchukuwa mbegu za pamba na kulima kwa tija.
Luhahula ameyasema hayo leo Ijumatano Novemba 13, 2019 wakati akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali kitongoji cha Lutamla kijiji cha Msai kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania.
Ziara hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipo fanya ziara Wilayani hapo Oktoba 6, 2019 ambapo aliagiza kutumia siku 4 kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuwaelimisha mambo mbalimbali yanayopatikana katika kila sekta na namna ambavyo watakavyoweza kunufaika kupitia sekta hizo.
Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wananchi kupanda kitaalamu ambapo hekari moja iwe na mashina 22,000 kwa mbegu ya pamba huku mbegu ya mahindi ifike mashina 18,000.
Luhahula amepongeza uuzaji wa pamba kuwa mzuri Wilayani hapo hali ambayo iliwafanya watu kutoka na Wilaya ya Meatu na Wilya ya Igunga kuja kuuza pamba, huku akiwataka wananchi kuwa na imani kuwa watalipwa fedha zao zilizobakia kwani Mnunuzi wa pamba alikuwa anadaiwa 700 milioni na sasa amebakiza 60 milioni ambazo Ijuma hii anakuja kuzimalizia.
Amewataka wananchi wa Mtoa kuacha vitendo vya kihalifu huku akiwatahadharisha mabalozi wote wanaoshindwa kuwabaini wanaotenda uhalifu katika maeneo hayo.
Halikadhalika amewataka wazazi kuwalinda watoto kutokana na vifo vinavyotokana na uzembe na kuwaonya wavulana na wanaume kuacha kuwachezea watoto wa shule na kuwapa mimba kwani hatua kali zitachukuliwa dhizi ya yule atakayempa mimba mwanafunzi.
“Mtoto wa shule ni wakwako kwa kuwa umemzaa lakini akiwa shuleni ni wakwangu mimi serikali, acheni kuelewana kupeana ng’ombe kwa mapatano ya waliowatia mimba wanafuzi,” amesisitiza Luhahula
Kwa upande wa afya Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa inayowawezesha kutibiwa wilaya yoyote Mkoani Singida kwa garama ya 30,000 tu kwa mwaka.
Akiwa ziarani hapo Mkuu wa Wilaya hiyo ameambatana na Maafisa mbalimbali waliotumia nafasi hiyo kuwaelimisha wananchi mambo mbalimbali.
Akiongea katika ziara hiyo Afisa Kilimo, Mwampashe Zawadi amewataka wananchi kufanya maandalizi ya kilimo kwa kusafisha mashamba, kuchoma masalia ya msimu uliopita na kuandaa pembe jeo.
Naye Afisa Afya wa Halmashauri hiyo, Salome Mwaipopo amewaagiza wananchi kuwa na vyoo vinavyoweza kuhimili masika, kiangazi, kuweka milango na paa katika vyoo hivyo.
Hatuwa hiyo itasababisha kutunza mazingira na kuepuka magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, homa za matumbo na mengineyo.
Akisisitiza suala la afya ya uzazi kwa wakinamama hao, Mwaipopo amewataka wakinamama wanaopata ujauzito kufika mapema kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya huku akiwataka wakinababa kuwasindikiza wakinama.
Kwa upande wake Afisa wa kuzuwia na kupambana na rushwa wilayani hapo, Benjamini Masyaga amewaelimisha wananchi rushwa ndogo na kubwa huku akiwataka kujiepusha nazo na kutoa taarifa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya jambo lolote la rushwa.
“ Rushwa ni fedha au kitu cha thamani anachopewa mtu mwenye madaraka ya jambo fulani ili mtoaji apate upendeleo” ameelimisha
Akibainisha madhara yatokanayo na rushwa katika jamii, Masyaga emeongeza kuwa rushwa inapokomaa hufanya maendeleo kutokuwepo na utu wa mtu kununuliwa.
Aidha amewataka wananchi kutambuwa jukumu lao la kusimamia fedha yoyote ya maendeleo itakayokuwa imeletwa kijijini hapo huku akiwata wadai kusomewa mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu na kutoa taarifa pindi viongozi wasiposoma mapato na matumizi.
Mkuu wa Wilaya hiyo amefanya ziara kijiji cha Msai na Masagi Wilayani humo.
Msai ni eneo maarufu kwa ulimaji wa pamba ambapo 2011 sherehe za pamba kitaifa zilifanyika hapo.
Afisa Kilimo Wilayani Iramba, Mwampashe Zawadi akifafanua mambo mbalimbali yanayohusu kilimo kwa wananchi wa Msai kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Afisa wa kuzuwia na kupambana na rushwa Wilayani Iramba, Benjamini Masyaga akielimisha mambo mbalimbali yanayohusu rushwa kwa wananchi wa Msai kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Afisa Afya Wilayani Iramba, Salome Mwaipopo akielimisha mambo mbalimbali yanayohusu afya ya uzazi, mazingira na CHF iliyoboreshwa kwa wananchi wa Msai kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Wananchi wa Msai wakifuatilia kwa makini wataalamu mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani hapo. Picha na Hemedi Munga
Wananchi wa Msai wakifuatilia kwa makini wataalamu mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani hapo. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.