Baraza la Biashara la Wilaya Iramba limefanyika Januari 31, 2025 katika Ukumbi Mikutano wa Halmashauri.
Baraza hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Suleiman Yusuph Mwenda na kuhudhuriwa na Wajumbe mbalimbali kutoka katika sekta ya Umma na sekta binafsi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo Mwenda ametoa wito kwa wafanyabishara Wilayani Iramba kuchangamkia fursa za Biashara Serikalini ikiwa ni pamoja na zabuni, ufundi ujenzi na nyinginezo. Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kuthubutu kuchukua mikopo ili kukuza Biashara zao.
"Tuna Mafundi wetu hapa.... tengenezeni nguvu ya pamoja unganeni ata Mafundi wa nne ili kutengeneza kampuni Moja nendeni kwa Afisa Biashara mkajisajili ili nanyi mpate fursa ya kushindania hizi kazi." amesema DC Mwenda
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bi. Magreth Segu ametumia Baraza hilo kueleza umuhimu wa Baraza la biashara ambao ni pamoja na uwepo wa jukwaa la majadililiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi,Wajumbe wa Baraza la biashara kujengewa uwezo wa kujenga na kutetea hoja, kuinua wigo juu ya upatikanaji wa Elimu juu ya masuala biashara, Elimu ya mlipa Kodi ujalisiliamali na uwekezaji na Baraza la Biashara kusaidia kubaini matatizo yanayoikabili sekta binafsi.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga Wilaya ya Iramba Bw.Abdala Tyenia ameiomba Serikali kuunga mkono umoja huo wa Wajasiliamali wadogo ili kuendelea kutoa kushirikiana kutoa Elimu kwa Wajasiliamali wadogo (Machinga) kuhusu umuhimu wa Kodi na namna Serikali ilivyo boresha mazingira mazuri kwao kibiashara katika suala Zima la ulipaji Kodi.
"Changamoto ambayo inatukumba sisi viongozi wa Wajasiliamali ni kwamba Wajasiliamali wengi na wamachinga bado hawajawa na elimu ya kutosha kujua kwamba Serikali imesha tengeneza mazingira rafiki ili waweze kufikia lengo la kuweza kulipa Kodi kupitia umachinga." Alisema Tyenia
Baraza hilo limejumusha Elimu ya Biashara kutoka kwa Afisa Biashara Wilaya Bw.Prosper Sostenes Banzi amabaye ametoa Elimu kwa Wajumbe kuhusu Shera ya Leseni za Biashara na Marekebisho Yake (Business Licensing Act No 25 of 972, Amendment 1980,2014 and 2015).
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.