Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Alhamisi Januari 30,2025 limeketi Mkutano wake wa kwanza wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya uliopo Mjini Kiomboi.
Mkutano huo wa Baraza umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kyengege Mhe. Innocent Msengi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya.
Akifungua mkutano huo Mhe. Innocent Msengi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Iramba Mbolea na Mbegu za ruzuku ambazo zimekuwa mkombozi kwa Wakulima Wilayani Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.