BARAZA LA MADIWANI IRAMBA LAPITISHA MAKISIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA TSH. BIL. 38.08 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Februari 14, 2025
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Iramba likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Innocent Msengi limepitisha Makisio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya kiasi cha Shilingi Bilioni 38.08.
Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 imewasilishwa na Afisa Mipango Bw. Fadhil Hassan kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri.
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imekadiria kukusanya na kutumia Shilingi Bilioni 38.08 ambapo Ruzuku ya Mishahara Shilingi Bilioni 21.8, Ruzuku ya matumizi mengineyo Shilingi Bilioni 2.06, Mapato ya ndani shilingi Bilioni 3.8, Miradi ya Maendeleo 5.2 na Wahisani - Miradi ya maendeleo shilingi Bilioni 5.08.
Baraza la Madiwani limepongeza waandaaji wa Bajeti hiyo kwa kuzingatia vipaumbele mahususi vilivyowekwa Kwa ajili ya Maendeleo ya Halmashauri wakiamini Miradi ya Maendeleo itatekelezwa na Wananchi watapata huduma Stahiki.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.