Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Baraza la Madiwani Wilayani Iramba, limemfukuza kazi Mtumishi wa Idara ya Afya, Muuguzi Daraja la tatu Rashidi Abed kwa tuhuma za kutokua kazini kwa zaidi ya siku tano.
Maamuzi hayo yametolewa leo Juni 2, 2020 na Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri Mjini Hapa.
Akitanganza maamuzi ya kikao cha kamati ya nidhamu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela amesama baada ya Baraza kujigeuza kuwa Mamlaka ya kinidhamu katika moja ya ajenda zake imemfuta kazi mtumishi huyo.
“Mtumishi Rashid Abed Muuguzi Daraja latatu ambae amepatikana na tuhuma ya kutokua kazini zaidi ya siku 5 na katika mahojiano na timu iliyomchunguza amedai kuwa hataki kufanya kazi Iramba,” amesema Tyosela na kuongeza
“Na sisi kwa mamlaka tulionayo tumemfuta kazi, hafanyi kazi Iramba na akatafute sehemu ambayo anahitaji yeye.”
Pia, kikao hicho kimewathibitisha kazi Wakuu wa Idara wawili, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dkt. Hussein Sepoko na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Jane N’gondi.
Halikadhalika, Kikao hicho kimepitisha jina la Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi ambalo limependekezwa.
“Tumepitisha jina ambalo limependekezwa la Mkurugunzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi, Ndugu Shiwariel Marunda.” Amesisitiza Mwenyekiti huyo na kutolea ufafanuzi
“Kikao kimewathibitisha kazini Watumishi saba wa kada ya utendaji wakata.”
Akiongea kwa njia ya Simu na Muandishi wetu, Mkurugenzi Mteule wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi, Shiwariel Marunda amewashukuru Wajumbe wote kwa kukubali kumteua kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi.
“Ninawashukuru Wajumbe wote kwa kuafiki mimi kupewa jukumu hilo ninaahidi nitatumika kwa kadri ya uwezo wangu kuitumikia Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na Taifa letu la Tanzania,” ameshukuru Marunda na kuongeza
“Kwa kweli tumepewa jukumu la kuhakikisha kwamba Wanairamba wanapata maendeleo na hasa tutajikita kutatua changamoto zao ambazo wamepewa Mji wanamatumaini kuwa zitaondoka.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni amewaomba Madiwani hao kuendelea kushirikiana kuhakikisha wanamaliza awamu hii ya uongozi salama.
“Baraza lako tukufu sina mashaka nalo kwa namna ambavyo tumeshirikiana katika miaka hii, hivyo niombe tuendelee kushirikiana ili tumalize vizuri.” amesema Mwageni
Naye Diwani wa Kata ya Shelui na Mwenyekiti wa Huduma za Jamii wa Halmashauri hiyo, Omary Kinota amewaomba Madiwani kuhakikisha wanawaeleza Wananchi waliopo katika maeneo yao kuhakikisha wanahifadhi chakula kwa kuwa baadhi ya maeneo hawakubahatika kupata mavuno mazuri kutokana na changamoto za mvua za mwaka huu.
Mkutano wa Baraza la Madiwani umefanyika leo na kuchakata dondoo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri na miradi ya maendeleo katika kata zote inakwenda vizuri.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akijibu maswali ya hapo kwa hapo toka kwa Madiwani Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakifuatilia hoja mbalimbali Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.