Hemedi Munga. Irambadc
Iramba. Baraza la Madiwani wilayani Iramba limemfuta kazi Mkuu wa Idara ya fedha, Muhidini Mohamed ambaye alikuwa Mweka hazina.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera katika ukumbi wa mkutano leo Septema 19, 2019.
Akitoa maamuzi hayo ya Baraza la Madiwani baada ya kujigeuza kuwa kamati ya mamlaka ya kinidhamu na kuchakata kwa kina mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera amesema kwa mamlaka ya baraza kutokana na makosa mbalimbali na makosa ya kitaalam kwa upande wa idara ya fedha baraza limemvua Mohamed madaraka yake na kumfuta kazi.
“ Lakini pia kwa masikitiko makubwa kwa makosa aliyoyatenda ya ubadhirifu na makosa mengine ya kitaalam kwa upande wa idara ya fedha Mkuu wa Idara bwana Muhidini Mohamed kwa masikitiko makubwa Baraza limemvua madaraka yake ya ukuu wa Idara na kumfukuza kazi” Alisema Tiyosera
Wakati huo huo Baraza limempunguzia adhabu bwana Julius Dyobili kwa kumpunguzia mshahara.
“Ninatangaza kwa mamlaka ya Baraza kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya bwana Julius Dyobili akiwa upande wa idara ya fedha kwa makosa yake aliyoyafanya Baraza limetoa adhabu ya kumpunguzia mshahara” Aliongeza Tiyosera
Hata hivyo Baraza limekamilisha uteuzi wa wakuu wawili wa Idara waliokuwa wakikaimu Idara hizo nakuwa wakuu wa Idara kamili ambapo Bibi Jeni Ngondi kuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ustawi Wajimii na Daktari Hussen Sepoko akiteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba Kiomboi.
Huku Baraza likikasimu madaraka ya ukuu wa Idara ambapo bwana Hadhil Ngayunga kuwa Mkuu wa Idara ya fedha yani Mweka Hazina na Bibi Tatu Ntandu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Ugavi wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Baraza pia limewathibitisha watumishi 59 kazini nakuagiza kuyafanyia kazi maamuzi yote yaliotolewa na baraza kwa mustakabali mzuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Akiongea katika baraza hilo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Iramba, Jamila Mujungu amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri na Baraza lake kwa ujasiri wa kutetea maslahi ya wananchi kwa upana wake.
Aidha amewapongeza madiwani na wataalam wote kwa hatua nzuri ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, huku akiamini kuwa watafika pazuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amewatoa hofu madiwani kuwa mahali ambapo panatarajiwa kujengwa stendi ya mabasi patakua na uwekezaji wa kisasa.
Huku akibainisha kuwa taratibu za kimanunuzi zitakamilika kwa haraka na mwezi wakumi mabasi yataanza kupita katika stendi hiyo ili kutengeneza chanzo cha mapato endelevu cha Halmashauri.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.