• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Baraza la Madiwani Wilayani Iramba limewafukuza kazi watumishi wawili wa kada tofauti

Posted on: March 13th, 2020

Hemedi Munga, Irambadc

tehama@irambadc.go.tz

Iramba. Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba limewafukuza kazi Watumishi wawili wa kada tofauti waliokuwa wakihudumu Wilayani hapa.

Maamuzi hayo yametangazwa leo Ijumaa Machi 13, 2020 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Simion Tyosela baada ya Baraza hilo kujigeuza kuwa kamati ya nidhamu katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.

“ Tulivyo jigeuza kuwa kamati ya  mamlaka ya kinidhamu Baraza letu tukufu limekubaliana kumfukuza kazi Mtendaji wa kijiji daraja la tatu  Yesaya Magala kwa tuhuma za rushwa,” amesema Tyosela

Magala anatuhimiwa kwa kosa la  rushwa na mahakama imemtia hatiani kwa kosa hilo kutokana na ushahidi wa kimazingira

Pia Baraza hilo limemfukuza kazi dereva daraja la pili, Juma Mgeni kwa kuto kuwa kazini kwa siku takriban 1460.

“ Baraza letu tukufu limeidhinisha kumfukuza  kazi Juma Mgeni kwa kuwa mfumo tayari umeisha muondoa,” amesema Tyosela

Halikadhalika Tyosela amewataka Madiwani wa Baraza hilo kuwaelimisha Wananchi waliopo katika maeneo yao kulima mazao ya muda mfupi ili mvua zitakapokata waweze kupata mazao na kuweza kuepukana na janga la njaa.

Akijibu swali la Diwani wa Kata ya Shelui, Kinota Hamisi aliyetaka kujua Mchango wa Wananchi katika ujenzi wa kituo cha Afya Shelui, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni amesema wananchi wanapaswa kushiriki na tayari wameanza kuwaelimisha namna ya ushiriki wao.

Mwageni amewaomba Madiwani hao kutoa elimu kwa wananchi wao kuchukua  tahadhari yakuweka miundombinu vizuri dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha huku akiahidi kuyafanyia marekebisho maeneo yatakayokuwa yameathirika.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Samwel Shillah amewashukuru  Madiwani hao kwa ushirikiano wanaoutoa katika kamati ya Fedha, mipango na Utawala huku akiwataka kuchukua vibanda vitakavyojengwa katika viwanja vya stendi mpya ya mabasi kijiji cha Misigiri Kata ya Ulemo.

Baraza la Madiwani lilianza kwa maswali ya papo kwa papo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuyatolea majibu.

Baraza la Madiwani hukaa kikao  chake cha kisheria kila baada ya miezi mitatu.

MWISHO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akijibu maswali mbalimbali yalioulizwa na Madiwani. Wakatikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Simion Tyosela na kushoto mwa Mwenyekiti huyo ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Samwel Shillah. Picha na Hemedi Munga

Madiwani wakisikiliza dua ya kuliombea Baraza ikisomwa  na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Simion Tyosela. Picha Hemedi Munga

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa za kamati mbalimbali za Baraza hilo. Picha na Hemedi Munga

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa za kamati mbalimbali za Baraza hilo. Picha na Hemedi Munga

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa za kamati mbalimbali za Baraza hilo. Picha na Hemedi Munga

Wenyeviti wa Kamati za Baraza hilo wakijiandaa kuwasilisha taarifa za kamati zao wakati wa kikao cha Baraza hilo. Picha na Hemedi Munga


Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • KIDATO CHA KWANZA KURIPOTI SHULE January 13, 2025
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI IRAMBA October 02, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"

    March 24, 2025
  • DC MWENDA AWASISITIZA WALIPA KODI KUFANYA MAKADIRIO YA KODI KABLA YA MACHI 31, 2025

    March 20, 2025
  • DC MWENDA NA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA WACHANGIA JUMLA YA MADAWATI 98 SHULE YA MSINGI MSANSAO ILIYOPO KATA YA MTEKENTE

    March 10, 2025
  • WALIMU WAKUU 108 WA SHULE ZA MSINGI NA MAAFISA ELIMU KATA 20 WILAYANI IRAMBA WAPEWA MAFUNZO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI FANISI KUPITIA JUMUIYA ZA KUJIFUNZA ZA WALIMU WAKUU NA MAAFISA ELIMU KATA

    March 19, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.