Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba limejadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi shilingi 38,088,278,131.59 kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Kikao hicho, kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Bw. Jeremia Kahuranga, kililenga kupitia na kutathmini utendaji kazi, huku wajumbe wakitoa maoni yao juu ya bajeti hiyo.
Baraza hilo limefanyika Februari 11, 2025 katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Fadhil Hassan kutoka Idara ya Mipango na Uratibu alieleza kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Pia, ofisi ya Mipango na Uratibu itaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya kikao hicho ili kuboresha huduma za kijamii na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi, ikiwemo TUGHE, TALGWU, CWT, pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri. Pia ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha uwazi na ushirikishwaji wa wafanyakazi na wadau mbalimbali katika mchakato wa kupanga na kutekeleza bajeti ya Halmashauri.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.