Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amewaagiza Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo Kiomboi kupanda miti ya matunda katika maeneo yao ya utawala.
Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu machi 9, 2020 wakati akiongea na Wajumbe hao katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
“Ninawaagiza kuhakikisha azimio la Baraza la Madiwani kuhusu kupanda miti ya matunda linatimizwa na nyinyi wajumbe wa Mamlaka ya mji mdogo kiomboi ili kuupamba mji ukae vizuri,” ameagiza Mwageni
Akiwajengea uwezo Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo Kiomboi, Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo, B’hango Lyangwa amewaambia kuwa wanatakiwa kuhakikisha kipindi cha uongozi wao wanapata uwekezaji wakutosha huku akiwataka kufahamu kuwa kulitekeleza hilo nikuingia katika historia ya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi.
Pia amewataka kufahamu kuwa uwepo wa wenyeviti wa vitongoji imara ndio utakosababisha Mamlaka hiyo kupata maendeleo.
“ Ninaomba mtambue kuwa mkiwa na ari ya maendeleo na wananchi walio katika maeneo yenu watapata maendeleo,” amesema Lyangwa na kuongeza
“Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi haiji kufuta vitu vizuri ispokuwa inakuja kuviimarisha,”
Halikadhalika amewataka wajumbe hao kuifahamu mipaka ya maeneo yao itakayowawezesha kutekeleza majukumu ya kudumisha na kuimarisha amani na utulivu, kuendeleza uchumi endelevu na kuwashauri wakazi waliopo ndani ya maeneo yao, kuanzisha mipango miji kwa maendeleo ya maeneo yao, kuhamasisha jamii kupambana dhidi ya adui maradhi, ujinga na umasikini, kutunga sheria ndogo, kutoa kodi na kutoza ushuru na garama mbalimbali.
Naye Afisa Mipango Miji wa Halmashauri hiyo, Valerian Msigala amewataka Wajumbe hao kufahamu kuwa ardhi hupanda thamani katika Mamlaka ya Mji mdogo, hivyo wanapaswa kutambua maeneo watakayo yauza yamepangiwa mpango gani katika mpango mji ili kuepusha migogoro.
“ Niwaondoe hofu kuwa huko tunakoelekea ni pazuri kuliko tulipotoka,” amesisitiza Msigala
Kwa upande wake mjumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo Kiomboi, Enock Duke ameushauri uongozi wa Halmashauri hiyo kufikisha elimu walioipata kwa wananchi ili kuwarahisishia wajumbe hao utekelezaji wa majukumu yao mjini hapa.
Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi ilitangazwa na Tangazo la Serikali Na, 301 la Agasti 22, 2014.
MWISHO
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi wakijadili muundo na kazi za wajumbe wa Mamlaka hiyo. Picha na Hemedi Munga
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi wakiwasilisha muundo na kazi za Mamlaka hiyo. Picha na Hemedi Munga
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kiomboi wakifuatilia mada zinazohusu kazi na muundo wa Mamlaka hiyo. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.