Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wamefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa Lengo la kujifunza kuhusu zao la alizeti linalolimwa Wilayani hapo.
Ziara hiyo ya Mafunzo imefanyika Disemba 03,2024 katika kata ya Mtoa, kata ya Shelui pamoja na kata ya Ulemo. na imeambatana na mafunzo yanayo husu upatikanaji wa Mbegu Bora za Alizeti, Elimu ya Ugani, uandaaji wa mashamba, masoko, Viwanda vya kusindika, Wajasiliamali wa Mafuta, Vikundi vya Wajasiliamali wa Bidhaa zinazotokana na zao la Alizeti. Pia imehusisha kuwatembelea baadhi ya wakulima wa zao hilo katika kata ya Mtoa.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa mapokezi uliyofanyika Katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Iramba Innocent Msengi ameshukuru ujio wa ugeni huo na ametoa wito kwao kuyafanyia kazi mafunzo hayo ya zao la Alizeti.
"Mkurugenzi na mwenyekiti kuchukua maamuzi ya kuja Iramba mmetuheshimisha. Mwaka 2014 Tumewahi fika pia Masasi, tulifika kujifunza namna ya kukusanya kwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani. Niwaombe hiki tutakachojifunza tuweze kukitumia." Amesema Innocent Msengi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ibrahimu Issa Chiputula amemesema ziara hiyo ya mafunzo ina lengo pia lakujifunza kuhusu mapato ili kurahisisha utekelezaji wa Miradi ya Wananchi na kutatua Kero zao.
"Ndugu zangu tumekuja kwaajili ya mapato. Halmashauri yenye mapato ndiyo Halmashauri ambayo itakuwa na nguvu ya kutekeleza Miradi ya Wananchi na kuondoa Kero za Watanzania. Kwahiyo tumekuja kujifunza kwenda kuongeza kwenye kipande hicho tulicho nacho, tukiongeza na Yale mtakayo tupatia nasi twaweza songa mbele. Amesema Ibrahimu Chiputula
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Bwana Michael Matomora ameshukuru ujio wageni hao na ameahidi kuwapa ushirikiano katika mafunzo kupitia kwa wataalamu wa Kilimo wa Halmashauri.
Alizeti ni zao la Biashara Wilayani Iramba. Zao hilo hulimwa katika kata zote zikiongozwa na kata ya Mtoa ambayo hulimwa zaidi. Zao hilo linachangia katika upatikanaji wa Mafuta ya kula ndani na nje ya Wilaya.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.