DAS MWAKIBETE ASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO YA JADI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025
Fainali ya Bonanza la Michezo ya Jadi ilifanyika Stendi kuu ya Mabasi Kiomboi Oktoba 25-26, 2025 ikiwakutanisha mashabiki wa michezo ya bao, drafiti na karata kwa burudani na ushindani.
Tukio hilo lililenga kuimarisha umoja, kuenzi michezo ya Jadi na kuhamasisha wachezaji wa michezo hiyo kujitokeza kupiga kura siku ya Uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba 29, 2025.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Bi. Bupe Mwakibete alitoa wito kwa wachezaji na mashabiki wa michezo Iramba kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa maendeleo ya michezo na nchi kwa ujumla.
"Nitoe wito kwenu kwamba, ili tupate viongozi sahihi wa kuendeleza michezo na maendeleo mengine katika Wilaya yetu na kitaifa kwa ujumla, tuchague viongozi ambao ni sahihi na wenye maono mema. Na tuhamasishane kutunza amani." Alisema Bi. Mwakibete.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Michezo Wilaya Ndg. John Mghana aliwapongeza wachezaji na mashabiki wote waliojitokeza katika michezo hiyo akiwasisitiza kuenzi michezo ya Jadi.
Bonanza hilo liliongozwa na kauli mbiu isemayo “Michezo ya jadi ni urithi wetu – tuienzi, tuifurahie!” lilishindanisha wachezaji wapatao 48 kutoka vituo vya michezo ya jadi 4. Takribani mashabiki 140 walijitikeza.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.