Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mzee wa miaka 87 ayakumbuka mazuri ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mzee huyo alietambulika kwa jina la Daudi Mlundi, mkazi wa kitongoji cha Kilundo kata ya kiomboi, Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania amesema Mwalimu Julius Nyerere alisema binadaam wote ni sawa.
Mlundi aliyasema hayo leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 Kilundo wakati akiongea na M wandishi wetu kuelekea kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Binaadam wote ni sawa hakuna ubaguzi, na wala usibague rangi, hii inatokana na kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa mpezi wa binaadam wote wala hakubagua. Tajiri na masikini, aliosoma asiesoma hakuwaweka mbali. Aliongeza Mlundi
Anachokikumbuka Mlundi, wakati alipoteuliwa kuwa balozi wa kitongoji cha Nzega ambacho kwa sasa kinaitwa Nnguluko alipewa kitabu kilichokuwa kimeandikwa kuwa “ Binadaam wote ni sawa hakuna ubaguzi”
Huku akifafanua kuwa kitabu hicho alikuwa anapewa balozi ili wasibaguane hata kama yeye ni balozi akae na watu wakiwa huru.
Mwalim Julius Nyerere akiwa Muadui Shinyanga 1961, aliwaamuru waafrika wakae kwenye viti na wazungu wakae chini. Alisimulia Mlundi
“Nyinyi wazungu kaeni chini na muafrika akae kwenye kiti” Alisema Nyerere
Akiongea na Mwandishi wetu, Mlundi amesema kuwa Mwalimu Nyerere aliwaambia wananchi wasichelewe kuota vitambi kwa kuwa tayari wako huru.
“Msichelewe kuota vitambi sasa hivi ni uhuru, sasa hivi mayayi mtakula nyinyi.” Alisema Nyerere
Hayo yalikuja baada ya kupata uhuru kwa kuwa kabla ya uhuru kipindi cha Muingereza mayayi walikuwa wakipelekewa Waingereza na Muafrika hakuruhusiwa kula mayayi.
Mlundi alieleza kuwa Mwalimu Nyerere alipendelea lugha ya Kiswahili kutumika katika viwanda huku akitolea mfano wa Kiwanda cha Sungura kilichoko Dar es salaam.
Mwalimu Julius Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.