Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amefungua rasmi Kongamano la ufunguzi wa Msimu wa kilimo 2024/2025 Kimkoa Ijumaa Novemba 1,2024 katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Kongamano hilo limewajumuisha wadau kadhaa wa kilimo na limehusisha uwepo wa mabanda ya utoaji wa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri, Upimaji wa Afya ya udongo, uuzaji wa Mbegu na Mbolea za Ruzuku, Viwatilifu, Chanjo kwa bei nafuu, usajili wa Wakulima kwenye mfumo wa pembejeo na Ruzuku ili kupata namba ya Mkulima.
Pia ufunguzi huo umeambatana na burudani mbalimbali pamoja mdahalo wenye mada kadhaa ikiwa ni pamoja na Ruzuku ya Mbolea na Mbegu za mahindi, Kilimo Cha mbaazi, Mfumo wa stakabadhi ghalani, Mifugo inalipa, Fursa za uwekezaji na Utalii katika Ziwa Kitangiri.
Kongamano hilo litahitimishwa Novemba 2, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.