Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amefurahishwa na Kasi ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Ishanga iliyopo Kata ya Shelui
DC Mwenda ametoa Pongezi hizo Juni 6,Mwaka huu kwenye ziara aliyoifanya shuleni hapo akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba pamoja na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali za serikali zilizopo Wilayani humo.
"Niwapongezs sana mafundi kwa kazi nzuri mnayofanya usiku na mchana kuhakikisha Mradi huu unakamilika kwa wakati" -alisema DC Mwenda
Aidha Mwenda ametoa Pongezi kwa Kamati zote zinazohusika na usimamizi wa Mradi huu kwa kuwa waadilifu na kukimbizana na Kasi pamojana tarehe ya kuhakikisha Mradi unakamilika kwa haraka kama ilivyopangwa
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.