DC MWENDA AHAMASISHA UZALENDO KWA WANAFUNZI KUPITIA MHADHARA WA KITAALUMA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameongoza Mhadhara wa Umahiri, Uzalendo na fursa kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Katala uliowashirikisha Wanafunzi wa Shule hiyo na Walimu
Dc Mwenda ameongoza Mhadhara huo Machi 18,2025 huku akitoka Pongezi kwa Walimu wa Shule hiyo kwa kuanzisha programu ambayo itachochea Uzalendo kwa Wanafunzi ili kufahamu kwa upana historia ya Tanzania kabla, wakati na baada ya ukoloni ili Wanafunzi waweze kufahamu historia na Mchango wa Viongozi mbalimbali nchini.
Hatua hii ya kuanzisha mihadhara ya kitaaluma imepongezwa na Mkuu wa wilaya na kuomba shule na vyuo vya kati viige mfano huo bora ili kupanua maarifa ya vijana.
"Mwaka 2017 tulifanya utafiti Jijini Dar es Salaam kufahamu ni kwa namna gani Wanafunzi wanafahamu kwa undani Mchango wa Viongozi mbalimbali Katika harakati za kupigania uhuru isivyo bahati, Tuliwauliza mnamfahamu Mwalimu Nyerere, Kawawa na Kambona, Wanafunzi wengi walishindwa kufahamu mchango wa Viongozi hao, tulipouliza nani anafahamu wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Wachezaji wa timu ya Simba na Yanga wote walinyoosha Mikono." Amesema DC Mwenda
Shule ya Sekondari Katala imeanzisha programu maalum ya mhadhara (public lecture) kwa lengo la kuchochea fikra yakinifu na mitazamo chanya katika nyanja mbalimbali za kijamii.
Aidha Katika uwasilishaji wake umeibua fikra yakinifu na tunduizi zenye kuhimiza uzalendo wa hali ya juu hasa kwa kizazi cha karne hii (generation Z and generation Alpha) ambao wanachochewa na ukuaji wa teknolojia. Na kwa namna nyingine athari kubwa ni kusahau Utamaduni wa jamii zao na kukosa uzalendo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.