Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda, amepongeza, hamasa inayofanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuzunguka nchi nzima kupitia kampeni ya 27 ya Kijani, yenye Lego la kupandamiti, kutunza mazingira na kufuatilia maendeleo ya mitiiliyopandwa.
DC Mwenda ametoa pongezi hizo Jumapili Julai 27 wilayani Iramba wakati akishiriki zoezi la upandaji miti 1000 lililofanikishwa na TBC Kama muendelezo wa kampeni hii ya ya kitaifa.
Kiongozi Huyo amesema Viongozi wa serikali wanaunga mkono kikamilifu jitihada za utunzaji mazingira, huku wakihamasisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.