Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda akimkabidhi pikipiki Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Milambo iliyopo Kijiji cha Mingela Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba, Mwalimu Hussein Kionda, kwa lengo la kuondoa changamoto ya usafiri inayomkabili Mwalimu huyo katika kutimiza majukumu yake ya kazi.
Mwenda ameyasema hayo Novemba 1,2024 wakati akimkabidhi pikipiki Mwalimu Hussein Kionda nje ya Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na Kaimu Afisa Elimu idara ya Elimu Awali na Msingi Agnes Peter
Aidha Mwenda amesema kuwa , kutokana na Changamoto kubwa ambayo ilikuwa inamkabili mtumishi huyo kutoka na ukosefu wa miundo mbinu ya Barabara na hakuna Usafiri wa Aina yoyote Unaoweza kufika Eneo hilo na hakuma huduma muhimu, ilimfanya mtumishi huyo kupata shida ya kufika na kufanya kazi zake ipasavyo.
"Malengo ya Wilaya ya Iramba katika Ufaulu ni kufika Asilimia 100 % na Kwa Sasa tupo kwenye Asilimia 77% hivyo tukio hili litakuwa Endelevu Kwa Shule zote na kuhakikisha kuwa tumeziondoa.Tumekuwa tukitoa Motisha kwa walimu na Wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma mwaka huu tulitoa Kompyuta kwa Kila Shule zilizofanya vizuri kitaaluma kwa Kata 20" Amesema DC Mwenda
Kipekee nimpongeze na Kumshukuru Afisa Elimu idara ya Elimu Awali na Msingi Mwalimu Rose Kibakaya,Amekuwa msikivu na Kila mara tumekuwa tukipanga mikakati ya Kuinua ufaulu kwa kuhakikisha tunatoka Motisha kwa walimu na Wanafunzi wanaofanya vizuri.
"Tunashirikiana na Wanafunzi wa Shule ya Vestfyns Efterskole iliyopo Mji wa Tomerrup
nchini Denmark wamefanya ziara ya Kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba kwa lengo la kukuza ushirikiano,Mwaka Jana walikuja Wilayani kwetu kujifunza mambo mbalimbali na Sisi tumepanga mwishoni mwa Mwaka huu tutawapeleka wanafunzi 25 na walimu na Wakuu wa Shule za Sekondari za Lulumba na Tumaini ziara Nchini humo ikiwa ni Mikakati niliyoiweka ya kuhakikisha Kila anayefanya vizuri atakuwa anapata Motisha" Amesema DC Mwenda
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.