DC MWENDA AONGOZA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA KILICHOWAKUTANISHA VIONGOZI WA WILAYA ZA IRAMBA,IGUNGA,MEATU NA KISHAPU
MKuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda ameongoza kikao Cha ujirani Mwema kilichowakutanisha Viongozi mbalimbali wa wilaya za Meatu mkoa wa Simiyu,Iramba- Singida,Igunga-Tabora na Kishapu- Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kunusuru ziwa Kitangiri ambalo lipo hatarini kupotea kutoka na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kwenye vyanzo vya ziwa na ndani ya ziwa hilo ikiwemo kilimo na ufugaji.
Ziwa hilo linatajwa kuwa na matope kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji.
Miongoni wa wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora ni wakuu wa wilaya,wakurugenzi,kamati za ulinzi na usalama za wilaya zote ,madiwani,Viongozi wa wafugajina wataalamu mbalimbali kutoka katika wilaya hizo nne.
Viongozi hao wamejadili namna ya kutengeneza uhifadhi na matumizi endelevu ya Bonde la Wembere na ziwa Kitangiri ambalo lipo katika mpaka wa mkoa wa Shinyanga,Simiyu,Singida na Tabora
Ziwa Kitangiri linapokea maji kutoka mto Manonga,Sanga,Sibiti,Semu,Ndurumo na Nzalala.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.