Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda leo tarehe 27 Novemba 2024 ameshiriki zoezi la uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa katika kituo cha Zahanati kata ya Kiomboi wilaya ya Iramba Mkoani Singida na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi wanao ona wana uwezo kuwaongoza.
DC Mwenda ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Zahanati ametoa wito kwa wananchi wote kufika kwenye vituo vilivyoandaliwa ili wapige kura na muhimu wachague viongozi ambao wanaridhika nao.
“Mara nyingi hatuendi kuchagua viongozi baada ya hapo wakishachaguliwa tunaanza kulalamika, basi kama Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyotuhamasisha wote akasema tusipoteze fursa hii… tuitumie fursa hii kuchagua viongozi ambao watatuletea maendeleo na kudumisha amani na usalama Katika maeneo yetu tunayoishi. Twende kupiga kura kuchagua viongozi ambao tunaona wanatufaa lakini pia tutekeleze wajibu wetu na haki yetu ya kikatiba,” amesema DC Mwenda.
Aidha Mwenda amewahakikishia Wananchi wa Wilaya ya Iramba kuwa hali ya Ulinzi na Usalama Iko shwari na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejipanga kuhakikisha uchaguzi unaenda Katika Hali la usalama amani kwenye Vituo Vyote 393 vya kupigia kura.
"Ulinzi Katika Vituo Vyote umeinarishwa na nitoe Rai kwa Wananchi wote wanaoenda vituoni kupiga kura wahakikishe wakimaliza kupiga kura wasibaki kwenye Vituo,Kwa yeyote atakaeleta fujo au kihatarisha amani vyombo vya ulinzi na usalama vitamchukulia hatua Kali za kisheria." Amesema DC Mwenda.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.