DC MWENDA APONGEZA UJENZI WA KARAKANA YA UFUNDI SHULE YA MSINGI LULUMBA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda, amepongeza ukamilikaji wa ujenzi wa Jengo 1 la karakana ya ufundi na matundu 2 ya vyoo wenye thamani ya shilingi milioni 54 uliopo Shule ya Msingi Lulumba, wenye lengo la Kuwawezesha vijana wa miaka kati ya 14 hadi 19 kujiajiri wenyewe kwa fani za ufundi ambazo ni Ushoni, Kilimo cha bustani na ufundi magari.
Mwenda ameyasema hayo Septemba 23, 2025, wakati akikagua ujenzi wa mradi huo baada ya kupokea taarifa ya mradi kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Jacob Omary, DC Mwenda alisema "Mradi huu unalenga kuwajengea uwezo wa ufundi vijana kwa kujifunza na kuongeza kipato chao".
Aidha, alisisitiza wataalamu wa Halmashauri kuendelea kutoa elimu ya Mfumo wa NeST kwa mafundi ujenzi waliopo katika Kata ya Shelui ili waweze kushiriki kikamilifu katika zabuni za kazi za ujenzi zinazotolewa na Serikali.
“Tuna mafundi wengi katika kila kata, waiteni waambieni tunahitaji mafundi kwa sababu tunajenga shule hapa. Waelekezeni namna ya kuomba kazi hizi, waelezeni faida na waelekezeni jinsi ya kuomba kazi hizi kwenye mfumo ili waanze kuomba na kufanya kazi”
Katika ziara hiyo ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, DC Mwenda alitembelea na kukagua ujenzi wa Majengo ya Shule ya mkondo mmoja na madarasa 2 ya elimu ya awali katika shule ya msingi Shelui yenye thamani ya shilingi milioni 348.2, ujenzi wa madarasa 2 Shule ya msingi Galangala, ujenzi wa vyoo matundu 5, kichomea taka zahanati ya Maluga, ujenzi wa shule ya Sekondari ya Amali Kijji cha Kitukutu, ujenzi wa matundu matatu ya vyoo shule ya Msingi Ulemo, ujenzi wa nyumba ya walimu Shule ya Msingi Ntwike. Ziara hiyo ililenga kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.