DC MWENDA ASISITIZA UDUMISHAJI WA AMANI TARAFA YA KINAMPANDA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025
IRAMBA, Oktoba 21, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda, amewataka wananchi wa Tarafa ya Kinampanda kuendelea kudumisha amani na mshikamano kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Amali Kitukutu, DC Mwenda alikutana na viongozi wa Dini, viongozi wa kimila, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji pamoja na wazee maarufu wa tarafa hiyo, ambapo alisisitiza umuhimu wa utunzaji na udumishaji wa amani iliyopo nchini.
“Amani ni jambo ambalo siku zote tumeendelea kuhimizana kwamba ni jambo muhimu kuliendeleza katika nchi yetu kwa maendeleo ya taifa letu. Tusiruhusu kwa namna yoyote ile tukio lolote lenye asili ya kuchochea au kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema DC Mwenda.
Aidha, aliwahimiza viongozi hao kuendelea kuhamasisha wananchi waliojiandikisha na wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, ili kutimiza haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.