Na Hemedi Munga
Singida - Iramba. MKUU wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amegiza makampuni yote yanayojishughulisha na ulinzi na usalama katika tasisi za serikali na binafsi waajiri askari ambao wamepata mafunzo ya jeshi la akiba.
Mwenda ameto agizo hilo leo Ijumaa Oktoba 22, 2021 wakati akiongea na askari walioko katika mafunzo ya jeshi la akiba Tarafa ya Kinampanda kata ya Ulemo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Uwepo wa usalama na amani katika Wilaya hii una sababisha wananchi kujishughulisha na mambo ya maendeleo kwa utulivu unaowafikisha katika mafanikio wanayoyatarajia.
“Haiwezekani kuwapa silaha watu ambao wanakwenda kulinda ofisi aidha ya serikali au binafsi watu ambao hawana mafunzo ya jeshi la akiba.” Alikataza Mkuu huyo wa Wilaya na kuongeza kuwa
“Wale waajiri wote wanaojishughulisha kufanya kazi ya ulinzi katika Wilaya hii lazima wahakikishe askari wao wamepitia mafunzo ya jeshi la akiba ambao watakuwa na weledi wa kutunza silaha, nidhamu, heshima na wanajuwa uaminifu wa kuzitunza silaha hizo.”
Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito wa kuhakikisha kuwa makapuni ya ulinzi yanaajiri vijana ambao wametia mafunzo ya jeshi la akiba.
“Ni lazima tuwaajiri vijana hawa ambao wameonesha uvumilivu katika mafunzo yao ya jeshi la akiba na kamwe sinta kubali katika Wilaya yangu kuwaajiri watu wasio kuwa na mafunzo, hivyo ni lazima tutoe kipaombele kwa vijana walioshiriki mafunzo haya.”
Halikadhalika, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa askari ambao wameonesha umakini wakupatia wakati wa kurenga shabaha.
Mshindi wa kwanza amepata shilingi 50,000, mshindi wa pili shilingi 30,000 na mshindi wa tatu shilingi 20,000.
Awali akitoa taarifa fupi ya mafunzo namna ambavyo askari hao wemeonesha umahiri na umakini, Staff Sagent (SSGT) Benard kihaumbi amesema kuwa askari wa kiume (MG) Almasi Hamisi emekuwa wakwanza katika zoezi la kufunga na kufungua silaha huku askari wakike (MGM) wakionesha uhodari na ushindi wa kurenga shabaha.
Aidha Kihaumbi amemuhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa askari hao wako makini, mahiri na wazima kuendelea na mafunzo yao.
“Ndugu Mkuu wa Wilaya nikuhakikishie kuwa askari hawa hakuna ambaye anaumwa, wako salama chini ya kamati ya kurenga shabaha yenye askari 13 inayoongozwa na Afande RG Matimiso.” Alisema SSGT Kihaumbi
Kwa upande mmoja wa askari hao, Almasi Hamisi amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuwatembelea kambini katika mafunzo na kuwapatia zawadi.
Hamisi alisema kuwa maagizo ya Mkuu huyo wa Wilaya yamewahakikishia kupata ajira punde badaa ya kumaliza mafunzo yao.
Kufuatia hali hiyo, Hamisi ametowa wito kwa vijana waliopo Wilayani Iramba kujiunga na mafunzo ya jeshi la akiba kwa sababu watapata weledi, ukakamavu, nidhamu na ajira itakayowawezesha kumudu maisha yao pamoja na kuiweka Wilaya yao katika hali ya usalama na amani muda wote.
Kwa upande Diwani wa kata ya Ulemo ambaye ni mmoja wa askari hao, Peter John amesema kuwa askari hao wanamorari na wameiva wako tayari kulitumikia Taifa.
Mafunzo hayo ya jeshi la akiba yalianza manamo mwezi wa saba 2021 na yako katika hatua za mwisho za kurenga shabaha.
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jeshi waandamizi wanaoendesha mafuzo ya jeshi la akiba Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga.
Askari wa jeshi la akiba wakifuatilia maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda punde alipowatembelea kambini. Picha na Hemedi Munga
Askari wa jeshi la akiba wakifuatilia maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda punde alipowatembelea kambini Wakwanzan kushoto ni Diwani wa kata ya Ulemo, Piter J. Peter. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.