DC MWENDA ATEMBELEA KITUO CHA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MISIGIRI
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda Jumatano Mei 21, 2025 ametembelea Kituo cha kuandikisha Wapiga Kura kilichopo katika ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Misigiri na kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linavyoendelea. Zoezi hilo linaenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
DC Mwenda amewasisitiza Wananchi ambao Bado hawajiandikisha au kuboresha taarifa zao kutumia muda uliobaki kushiriki kilamilifu katika zoezi hilo litakalo wawezesha kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2025.
Zoezi la Uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linafanyika kwenye mikoa 16 ambayo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma na Dar es Salaam. Mikoa mingine ni Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei, 2025 na vituo vinafunguliwa saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.