DC MWENDA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SHULE MPYA YA AMALI KITUKUTU
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda leo tarehe 21 Mei, 2025 ametembelea Mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Elimu ya Amali Kitukutu lengo likiwa kujionea maendeleo ya utekekelezaji wa mradi huo wenye Thamani ya Shilingi Billioni 1.6 unaotekelezwa Wilayani Iramba.
Mradi huo utakapokamilika utatoa Elimu ya amali ambayo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa ufundi na ujasiriamali kwa lengo la kumudu maisha yao, kushindana katika soko la ajira na kuchangia maendeleo ya Taifa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.