DC MWENDA ATOA WITO KWA KILA MWANANCHI ALIYEJIANDIKISHA KUSHIRIKI KUPIGA KURA SIKU YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025
IRAMBA, Oktoba 23, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda ametoa wito kwa wananchi walio jiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura Wilayani Iramba kwenda kupiga kura siku ya Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 nchini.
Mwenda ameyasema hayo Oktoba 23, 2025 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Shelui alipokuwa akizungumza na na viongozi wa Dini, viongozi wa kimila, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji pamoja na wazee maarufu wa tarafa ya Shelui, ambapo alisisitiza umuhimu wa kupiga kura na kuendelea kudumisha amani.
“Twendeni tukahasishane kila mmoja kwa nafasi yake, tukawaambie watu tunawaongoza wote waliojiandikisha wakapige kura. Ukimaliza kupiga kura endelea na shughuli zako. Tuwahamasishe vijana kwamba twendeni tukalinde amani,” alisema DC Mwenda.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Bi. Bupe Mwakibete amesema kupiga kura ni haki ya kila mwananchi kikatiba ili kumchagua Kiongozi anayeona anafaa kwa maendeleo endelevu na mwenye kudumisha amani.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nselembwe Said Tyuni amempongeza DC Mwenda kwa kuwatembelea viongozi hao huku akiahidi kuendelea kuwahamasisha Wananchi kijijini hapo kulinda amani.
DC Mwenda aliambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya katika mkutano huo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.