• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Comments |
Iramba District Council
Iramba District Council

The United Republic of Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Iramba District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

DC MWENDA ATOA WITO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUIMARISHA UFUNDISHAJI KWA MADARASA YA MITIHANI

Posted on: May 6th, 2025

DC MWENDA ATOA WITO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUIMARISHA UFUNDISHAJI KWA MADARASA YA MITIHANI


Singida, Mei 6, 2025


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda, amewahimiza walimu wa shule za msingi wilayani humo kufundisha kwa bidii madarasa yanayotarajia kufanya mitihani ya kitaifa, ili kuendeleza mwenendo chanya wa ufaulu wa wanafunzi katika wilaya hiyo.


Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Iramba, Mwenda alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana mwaka 2024 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ilishika nafasi ya 8 kitaifa katika shule zilizoongeza ufaulu wa darasa la saba nchini, ikiwa imeongeza ufaulu kwa asilimia13.


"Tunapaswa kuendeleza rekodi ya matokeo mazuri katika Wilaya yetu. Fundisheni kwa juhudi zote Madarasa yenye Mitihani ya Kitaifa ili mwaka huu pia tuendelee vunja rekodi ya kuongeza ufaulu pamoja na kupata matokeo mazuri." Amesema DC Mwenda


Katika ziara hiyo, DC Mwenda pia aliwapongeza wananchi wa Iramba kwa kujitolea nguvu kazi kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


“Nawapongeza sana wananchi wa Iramba kwa moyo wenu wa kujitolea. Katika kila eneo nililopitia, nimekuta mwitikio mkubwa wa wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo. Hili ni jambo la kupongezwa sana na kujivunia,” aliongeza DC Mwenda.


Katika ziara hiyo, DC Mwenda alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Iramba ikiwemo: ujenzi wa ukamilishaji bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kidaru (Thamani: Shilingi milioni 60), ujenzi wa matundu 10 ya vyoo Shule ya Msingi Kidaru (Shilingi milioni 17), ujenzi wa matundu 10 ya vyoo Shule ya Msingi Tyegelo (Shilingi milioni 17), ukamilishaji wa Kituo cha Afya Tyegelo (Shilingi milioni 150), ujenzi wa matundu 10 ya vyoo Shule ya Msingi Luono (Shilingi milioni 17), ujenzi wa Shule ya Msingi Nkokilangi (Shilingi milioni 250), ujenzi wa Zahanati ya Mseko (Shilingi milioni 250), mradi wa ufungaji wa mfumo wa gesi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Shelui (Shilingi milioni 27.7).


DC Mwenda aliongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.


Announcements

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 02, 2026
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI June 05, 2025
  • View All

Latest News

  • MAONESHO YA MATUMIZI YA PEMBEJEO ZA KILIMO (MBEGU, MBOLEA NA VIUATILIFU) HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA DISEMBA 29-30, 2025

    December 28, 2025
  • HERI YA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2026

    December 25, 2025
  • DC MWENDA AWATAKA WALIMU IRAMBA KUONGEZA UBUNIFU NA BIDII KUINUA UFAULU

    December 09, 2025
  • HERI YA MIAKA 64 YA UHURU WA TANZANIA BARA

    December 09, 2025
  • View All

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
More Videos

Quick Links

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Related Links

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    KIOMBOI, IRAMBA

    Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Telephone: 026 - 2532253

    Mobile: 026 - 2533001

    Email: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.