Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amewapongeza viongozi mbalimbali kwa hatua walioifikia ya ukamilishaji wakuweka vibao vya Anwani za Makazi katika taasisi, mitaa, barabara na nyumba.
Mwenda ametoa wito huo leo Jumamosi Aprili 30, 2022 alipofanya ziara ya kukagua ukamilishaji wa kuweka vibao vya Anwani za Makazi katika kila mtaa, barabara, nyumba na taasisi wilayani hapa.
“Kwa kweli hongereni sana kwa sababu kazi hii mnayoifanya inarizisha, hivyo hakikisheni wakati mnaendelea kuchonga vibao hivi mnachimba na mashimo kwa ajili ya kusimika nguzo za kuwekea vibao.” Alisema
Aidha, aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitoa takribani Tsh 28 bilioni kwa ajili ya zoezi hili nchi nzima, hivyo fanyeni kazi mkijua kuwa kipo mtakachokipata.
Ninawashukuru sana na kuwaomba kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati kwa sababu swala hili lina tarehe ya mwisho ya ukamilishaji wake.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza viongozi hao kufanya manunuzi ambayo yanakuwa na risiti za mfumo wa kielektroniki.
Kwa upande wao mafundi waliopata tenda ya kutengeneza vibao hivyo wamekuwa na imani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuagiza swala ambalo limewapatia kipato na kufanikiwa kuendesha maisha yao.
Akiongea katika ukaguzi huo mmoja wa mafundi wanaochonga vibao hivyo, John Martin alisema kuwa Mfumo wa Anwani za Makazi umewafanya wao kutambulika na kuwa rahirisi kusafirisha samani mbalimbali wanazozitengeza katika mikoa na wilaya za jirani nchini.
“Kwa kweli ilikuwa ngumu kwa watu kufahamu siye mafundi tunapatikana wapi na tunaujuzi gani lakini kwa Mfumo wa Anwani za Makazi imekuwa rahisi siye kufahamika.” Alisema
Halikadhalika, alimpongeza Rais Samia kwa namna ambavyo aliagiza zoezi hili lifanyike ni maono ya hali ya juu ambayo yanafanikisha vijana kujipatia ajira za muda na zakudumu.
“Rais Samia ameturahisishia kupata wateja baada ya zoezi hili kuwepo tunafanya kazi kwa kujiamini na kutambua wateja wapo.”
Naye Alekzanda Martin alisema kuwa kazi hizi zimefanya wanaweza kukidhi mahitaji yao, hivyo alitoa wito kwa jamii kuendelea kuwaamini na kuwapa tenda zao.
Aliseama kuwa wao wanampongeza Rais Samia kwa sababu kama sioyeye kuagiza kutekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi wasingepata riziki hiyo.
Aidha, wanamuomba Rais Samia kuwaangalia mafundi seremala kwa kuwapatia mashine zitakawasaidia kurahisisha utendaji kazi wao na kuzalisha samani kwa wingi.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.