DC MWENDA AWASISITIZA WALIPA KODI KUFANYA MAKADIRIO YA KODI KABLA YA MACHI 31, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Walipakodi Wilayani Iramba kujitokeza kufanya makadirio ya kodi kabla Machi 31, 2025.
Mwenda ameyasema hayo Machi 20, 2025 wakati alipotembelewa ofisini kwake na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Mkoa wa Singida na Wilaya ya Iramba wakiongozwa na Meneja wa Mamlaka hiyo Mkoa wa Singida Bw. Josephat Mwaipaya
"Hongereni TRA mmekuwa mkikusanya Kodi Wilayani Iramba bila kutumia nguvu kwa Wafanyabiashara, wamekuwa wakiitikia wito bila shuruti nikupongeze CPA Iddi Omari Iddi, Najua Sasa hivi unamajukumu mapya ila Nina Imani kubwa ya Uliyemkabidhi Ofisi ataendeleza pale ulipoishia." Alisisitiza DC Mwenda.
Aidha Mwenda amewataka Maafisa hao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka Ofisi ya Mkoa na Wilaya ya Iramba kuendeleza kampeni ya elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango. Pia kuwasisitiza Wafanyabiashara kutoa risiti za EFD na wanunuzi kudai risiti wakati wote wanaponunua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.